MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amewahimiza watanzania kuendelea kuamini chama hicho kwani wametekeleza miradi kwa mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita.
Hayo amesema jana katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza kwenye ufunguzi wa kampeni za chama hicho katika kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ambapo alieleza kuwa mafanikio hayo yamewezesha kuaminiwa kuendelea kuongoza baada ya watia nia wa nafasi ya udiwani kata 91 kupita bila kupingwa.
Alisema kuaminiwa kwa chama hicho kunatokana serikali kutekeleza miradi ya maendeleo kwa mafanikio makubwa kwenye sekta mbalimbali mkoani hapo ambapo ujenzi wa miradi ya barabara kwa kiwango cha lami katika maeneo mbalimbali sehemu hiyo imewafurahisha wananchi katika eneo hilo.
Vilevile alisema kuwa ujenzi wa madarasa na miundombinu katika shule za msingi na sekondari, kukamilika kwa daraja la Magufuli lenye urefu wa zaidi ya kilomita 3 juu ya ziwa victoria kuwa vitu vinavyowakosha wananchi kuendelea kuaminiwa kwani kwa sasa wanachama zaidi ya milioni 13.3 wameandikishwa.
Dk Nchimbi ambaye alikuwa mlezi wa mkoa huo alisema serikali watakayoiongoza siku 100 wakiwa madarakani watahakikisha kuwa Bima ya Afya kwa wote inaanza kipaumbele cha awali kikiwa kwa mama wajawazito, watoto, walemavu na wazee.
Aliongeza kusema kuwa kwa upande mwingine wa sekta ya afya watazuia marufuku ya kutokuchukua maiti hospitalini kwa watu ambao hawajalipia matibabu ya marehemu.
Dk Nchimbi amesema ndani ya siku 100 serikali watakayoiunda itahakisha kuwa ajira 5000 kwenye utumishi wa umma zinapatikana kwa vijana wa kitanzania, jijini Mwanza uwanja wa ndege wa kimataifa kukamilika, ujenzi wa reli ya kisasa kati ya Isaka na Mwanza pia utakamilika.
Aliwaomba wananchi katika majimbo ya uchaguzi ya Nyamagana kumuchagua John Nzilanyingi na Ilemela Wlliam Kafiti kwa nafasi ya ubunge huku akiwaasa kuchagua madiwani wa CCM ili waweze kuharakisha jitihada za kuwaletea wananchi maendeleo.
Dk Nchimbi aliendelea kuwaomba watanzania kudumisha misingi ya amani na utulivu uliopo hapa nchini ili wananchi waendelee na shughuli zao za kimaendeleo katika maeneo yao.
GUSA LINK HAPA CHINI👇
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment