" Mahakama Kuu Yatupilia Mbali Kesi ya Kupinga Uteuzi wa Rais Samia

Mahakama Kuu Yatupilia Mbali Kesi ya Kupinga Uteuzi wa Rais Samia

 

Mahakama Kuu ya Tanzania kupitia Masjala Kuu ya Dodoma, Agosti 22, 2025 imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyokuwa ikipinga uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Kesi hiyo iliwasilishwa na Dkt. Godfrey Malisa, mkazi wa Moshi, dhidi ya Wadhamini wa CCM na Katibu Mkuu wa chama hicho.

Jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Joachim Tiganga, na kuhusisha Majaji Everisto Longopa na Griffin Mwakapeje, lilibaini dosari kadhaa za kisheria ikiwemo ukiukwaji wa masharti ya Katiba, kutokufuata taratibu za uchaguzi ndani ya CCM, pamoja na upungufu katika nyaraka za kiapo.

Miongoni mwa kasoro zilizojitokeza ni tofauti za majina ya mlalamikaji katika nyaraka zilizowasilishwa, hali iliyotia shaka uhalali wa kiapo hicho.

Kutokana na mapungufu hayo, mahakama iliamua kesi hiyo haina msingi thabiti wa kisheria na hivyo ikaifuta rasmi.


GUSA LINK HAPA CHINI👇


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post