Waumini wa kanisa la Tanzania
assemblies of God (TAG) Mbeya Forest ya kwanza wamehimizwa
kutokata tamaa katika maisha badala yake wajikite katika ibada na kumcha Mungu.
Akiongoza ibada hiyo iliyofanyika
kanisani hapo Agosti 31,2025 mtumishi wa Mungu Mchungaji Thobias Tambikeni
ameeleza athari za kukata tamaa na kuwa hali hiyo inawatokea waumini
pale majibu yanapochelewa.
Mchg Tambikeni amesema kuwa kukata
tamaa ni mbaya kwani hali hiyo husababisha mashabulizi kuwa mepesi muno kwani
adui shetani anapenya kwa haraka ambapo pia amewataka waumini hao kutambua kuwa Ile kazi ya uumbaji Mungu angeikatia
tamaa uumbaji huo ungeishia hapo.
Akitaja Athari nyingine za kukata
tamaa mtumishi huyo amesema kuwa ni kuangamia kabisa kiroho na kimwili, hivyo
licha ya waumini hao kukutana na misukosuko mingi
inayokatisha tamaa hawatakiwi kukata tamaa kabisa.
Akitaja Dalili za kukata tamaa amesema
kuwa mtu aliyekata tamaa ujitenga na wengine, hujikatia tamaa
na kujichukia au kujinyanyapaa mwenyewe akidhani anasemwa na wengine.
Aidha amesema Mungu hajawahi kushindwa
wala kuchoka hivyo ni wakati wa kuinuka.
Amesema kuwa hali ya kukata tamaa
imelitesa kanisa la sasa hivyo waumini wanatakiwa kutambua kuwa Bwana Yesu analeta
matumaini na faraja kwa haraka.
Mchungaji Tambikeni amewahimiza
waumini hao kujipa moyo kwani kazi ya Bwana ni kuleta matumaini.
Hata hivyo amewashauri waumini
kumfanyia Mungu ibada kwani matumaini ya mtu yanapotea pale mtu
unapoonyesha dalili za kukata tamaa hivyo wasilie wala wasichoke maana katika
mazingira hayo shetani huwapitia.

Post a Comment