" NISHIKE MKONO NITABASAM KUNDI NAMBA MBILI YAJA KIVINGINE MBEYA

NISHIKE MKONO NITABASAM KUNDI NAMBA MBILI YAJA KIVINGINE MBEYA

Na Lydia Ezra Lugakila MbeyaTaasisi ya nishike mkono nitabasam yenye lengo la kuisaidia jamii  imefanya kikao kikubwa ambacho kimeenda kuunda umoja huo nambari mbili kwa Mbeya ambapo umoja  nambari moja una miaka mitatu sasa na una Wanachama wasiopungua 600 na una makao yake makuu Tunduma Mkoani Songwe.Umoja huo nambari moja kutoka Taasisi ya nishike mkono nitabasam tayari umezaa matunda mengi katika jamii huku umoja nambari mbili ukiwa umeanzishwa Agosti 30 na kuwakusanya wanachama zaidi ya 100 ambao unakwenda kuisaidia jamii katika masuala mbali mbali ya furaha na huzuni na kuwasaidia wanachama  wenyewe kwa wenyewe pale inapotokea mmojawapo amepatwa na majanga.Akizungumza katika kikao cha ufunguzi rasmi wa kikundi namba mbili uliofanyika Agosti 30,2025 katika ukumbi wa Mfikemo hotel Sai jjijini Mbeya Mwenyekiti wa Taasisi hiyo  David Daniel Mwasimba amesema kuwa matatizo huwa hayabishi hodi hivyo ni vyema wanaumoja huo wakashikna na kusaidiana katika shida na hasa kuisaidia jamii inayowazunguka." Hakuna ambaye anajiandaa na matatizo yanapotokea watu wengi wamekuwa wakipata shida ikiwemo ugonjwa na misiba na wanashindwa pa kukimbilia hivyo tukijipanga katika hili tutafika mbali na kupanua familia hii kwa ajili ya jamii"alisema Mwasimba.Amesema kuwa taasisi ya nishike mkono nitabasamu katika kikundi nambari moja imekuwa ikifanya makubwa katika jamii tangu kuanzishwa kwake mnamo Desemba 25, 2022 ambapo umoja huo kikundi namba moja kinakwenda sasa mwaka wa tatu ambapo malengo yake ni kuisaidia jamii.Mwasimba taasisi hiyo pia imekuwa ya mfano kwani imekuwa ikijikita pia kupinga vitendo vya ukatili katika jamii, kugawa taulo za kike shuleni pamoja na kujitoa kwa watu wenye ulemavu kwani tayari baadhi ya wenye uhitaji wamejengewa nyumba.Amesema taasisi hiyo imesajiliwa kisheria kutoka Halmashauri ya mji wa Tunduma ambapo amewahimiza watu kuendelea kujiunga zaidi katika kundi namba mbili ili kusaidiana katika mambo makubwa.Aidha Wanachama hao walikutana kutoka sehemu mbali mbali za Mbeya Uyole, Tunduma,Tukuyu, mbalizi, ituha pamoja na maeneo mbali mbali ambapo wamewekeana mikakati mizuri ya kuanzisha umoja huo ili kuendelea kusaidia jamii na kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.Kwa upande wake makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya nishike mkono nitabasam Mwajuma Masoud amesema kuanza rasmi kwa umoja huo kutaruhusu mipango mingi kutokana na malengo  waliojiwekea hivyo watafika mbali zaidi huku akisisitiza Wanachama wengi kujiunga ili wafanye makubwa zaidi.Hata hivyo kwa upande wa baadhi ya wanachama hao wanaounda umoja huo akiwemo Faraja Luvanda, Lucy Kittu wameahidi kuwahamasisha wengi kujiunga huku wakitegemea makubwa zaidi.

GUSA LINK HAPA CHINI👇


APPLICATION FORM

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

 

Post a Comment

Previous Post Next Post