Mitandao ya kijamii imefurika na tetesi nzito kuhusu kifo cha Rais wa Marekani, Donald Trump, hali iliyozua mjadala mkubwa ndani na nje ya Marekani. Hashtag kama #TrumpIsDead na #TrumpNoMore zimekuwa zikisambaa kwa kasi kwenye majukwaa mbalimbali kama X (zamani Twitter), TikTok na Facebook. Tetesi hizo ziliibuka zaidi baada ya Makamu wa Rais, JD Vance, kutoa kauli tata katika mahojiano na USA Today kwamba yuko tayari “kuchukua nafasi endapo janga baya litampata Rais.” Kauli hiyo imechochea minong’ono kwamba kuna jambo kubwa linajificha kuhusu afya ya Trump.
Kuchangia zaidi kwenye uvumi huu, Rais Trump amekuwa mbali na macho ya umma kwa siku kadhaa, jambo ambalo ni nadra kwake kwani kwa kawaida huwa ni mtu anayependa kuonekana hadharani na kujihusisha kwenye mijadala ya kisiasa kila mara. Zaidi ya hapo, picha zilizovuja hivi karibuni zikimuonyesha akiwa na jeraha au alama ya kovu mkononi, zimezua hisia kwamba huenda ana matatizo ya kiafya yanayofichwa na Ikulu ya White House.
Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya siasa za Marekani wanasema uvumi huu unapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari kubwa. White House haijathibitisha taarifa yoyote kuhusu hali mbaya ya afya ya Rais, na kwa kawaida viongozi wa Marekani huwekewa ulinzi mkali wa taarifa za kiafya. Baadhi ya wachambuzi wanasema jeraha lililoshuhudiwa mkononi huenda ni alama ya kawaida kutokana na matibabu madogo kama sindano au kipimo cha damu, si lazima iwe dalili ya hali mbaya kiafya.
Hata hivyo, kwa upande wa kisiasa, tetesi hizi zinaongeza mvutano. Makamu wa Rais JD Vance anaonekana kujiweka tayari kisiasa kwa hali yoyote, jambo linalofasiriwa na wachambuzi kama kuashiria migawanyiko ndani ya utawala wa Trump. Wafuasi wake wanahofia kwamba tetesi hizi huenda ni sehemu ya kampeni za upotoshaji za wapinzani wake kisiasa.
Kwa sasa, swali kubwa linasalia: Trump anaendelea na afya njema lakini anajificha kimkakati, au kuna ukweli nyuma ya tetesi hizi? Wakati majibu rasmi yakisubiriwa, uvumi tayari umefanikiwa kutikisa mitandao na kuongeza mshindo wa kisiasa nchini
GUSA LINK HAPA CHINI👇
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment