Na: Dkt. Reubeni Lumbagala, TangaTume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetoa ratiba ya shughuli muhimu kuelekea katika zoezi la Kitaifa la Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025. Katika ratiba hiyo, zoezi la kampeni linatarajiwa kuanza Agosti 28 na kumalizika Oktoba 28, 2025 ili siku inayofuata ya Oktoba 29, 2025, wananchi waweze kupiga kura.Katika muda huo wa miezi miwili, wagombea watawazungukia wananchi ili kunadi sera zao ili kuwashawishi wananchi wawachague katika kipindi cha miaka mitano ijayo yaani mwaka 2025-2030. Wananchi wanao wajibu wa kuwasililiza wagombea ili kuwa katika nafasi nzuri ya kufanya maamuzi sahihi kwa mustakabali mwema wa maendeleo katika maeneo yao wanayoishi.Kimsingi, katika zoezi la kampeni, fedha zinahitajika sana. Mahitaji makubwa ya fedha pamoja na mambo mengine, yanachagizwa na ukubwa wa nchi yetu na namna ilivyo muhimu kuwafikia wananchi kule walipo ili kunadi sera. Wananchi wana shauku ya kusikia sera za wagombea Urais, Ubunge na Udiwani ili kufanya maamuzi sahihi ya nani wamchague ili waweze kushirikiana nae katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.Kwa kuzingatia umuhimu wa raslimalifedha kuelekea katika kampeni za Uchaguzi Mkuu, Agosti 11, 2025, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, kiliweka wazi kusudio lake la kuandaa harambee maalum ya kukusanya fedha kutoka kwa wanachama wa CCM, wadau na wananchi. Hii inatokana na mahitaji makubwa ya fedha yaliyopo katika kufanikisha kampeni za uchaguzi ambapo mahitaji ya fedha ni Shilingi Bilioni 100. Agosti 12, 2025, katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam uzinduzi ulifanyika rasmi mbele ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan.Katika harambee hiyo ya kuichangia CCM, fedha kiasi cha shilingi bilioni 86.31 zilipatikana ambapo kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 56.31 ni fedha taslimu huku shilingi bilioni 30. zikiwa ni ahadi.Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ndiye mgombea Urais kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alichangia milioni 100 huku Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi akichangia milioni 50. Wadau na watu binafsi mbalimbali waliunga mkono mpango huo ambapo walichangia fedha nyingi.Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu, CCM inahitaji fedha za kutosha kuweza kuwafikia wananchi kule walipo ili kunadi Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2025-2030 ambayo imejaa mambo mazuri yenye kugusa maisha ya wananchi.Hivyo basi, wanachama, wapenzi, mashabiki, wakereketwa na wananchi kwa ujumla wanakaribishwa kuchangia fedha ili kukipa nguvu zaidi Chama katika kuwafikia wananchi.

Post a Comment