Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika – Tanzania (MISA TAN) imepongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kutimiza miaka 7 tangu kuanzishwa kwake.
MISA TAN imesema mafanikio yaliyopatikana katika kipindi hicho, ikiwemo ulipaji wa zaidi ya shilingi trilioni 11.96 kwa wanachama na makusanyo ya takribani shilingi bilioni 168.25 kila mwezi, ni ushahidi wa ufanisi wa mfuko huo katika kuhudumia wananchi.
Aidha, taasisi hiyo imesisitiza itaendelea kushirikiana na PSSSF na wadau wengine katika kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa maendeleo ya taifa.
Post a Comment