" MR. BLACK KUFANYA MAFUNZO YA TANZANIA SCHOOL TO SCHOOL TOUR MKOANI MTWARA

MR. BLACK KUFANYA MAFUNZO YA TANZANIA SCHOOL TO SCHOOL TOUR MKOANI MTWARA

 

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mwezeshaji maarufu na Mkurugenzi wa The True Life Foundation, Peter Frank maarufu kama Mr. Black, anatarajiwa kuendelea na ziara yake ya mafunzo iitwayo Tanzania School to School Tour chini ya mradi wa Youth Perspective Forum unaoendeshwa na The BSL Investment Co. Ltd kwa kushirikiana na The True Life Foundation.

Kwa mujibu wa ratiba, Mr. Black atakuwa mkoani Mtwara leo Jumamosi, Agosti 16, 2025, ambapo mafunzo yatafanyika katika Shule ya Msingi Sasurea kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana.

Mafunzo hayo yanalenga kujenga uwezo wa kijamii, kitaaluma na kiutu kwa vijana, walimu na wadau wa elimu kupitia mada mbalimbali muhimu zinazogusa taaluma na uongozi wa shule.

Mada zitakazojadiliwa katika mafunzo hayo ni pamoja na:

  1. Usimamizi wa Shule na Ujuzi wa Uongozi (School Management and Leadership Skills)
  2. Huduma kwa Wateja na Malezi ya Watoto (Childcare and Customer Care Skills)
  3. Maadili ya Walimu na Utaalamu (Teachers’ Ethics and Professionalism)
  4. Ubunifu wa Maudhui, Ujumuishaji na Uwasilishaji (Content Designing, Integration and Deliverance)
  5. Utendaji wa Shule, Uwekaji Chapa na Masoko (School Performance, Branding and Marketing)
  6. Michezo ya Kiingereza na Matamshi Sahihi (English Games and Pronunciation)

Kwa mujibu wa waandaaji, lengo la mafunzo haya ni kusaidia walimu na vijana kutambua nafasi yao katika jamii, kuongeza ufanisi wa kielimu, na kujiandaa kwa changamoto za soko la ajira na maisha ya kila siku.

Kwa maelezo zaidi au kushiriki katika ziara zijazo, wasiliana kupitia:
📞 0712 583 756 / 0752 849 726
📧 pblack969@gmail.com
📱 Instagram: @bslschools




Post a Comment

Previous Post Next Post