Na Mapuli Kitina Misalaba
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia
mwanamke aitwaye Pendo Samson Methuthela (37) mkazi wa Kata ya Masekelo,
Manispaa ya Shinyanga, kwa tuhuma za mauaji ya mwenza wake Timotheo Magesa (35),
fundi magari mkazi wa Masekelo, aliyefariki dunia baada ya kukatwa kwa kitu
chenye ncha kali kwenye mkono na tumboni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth
Magomi, amesema tukio hilo lilitokea Agosti 23 majira ya saa tatu na nusu usiku
katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Bashwee Lodge iliyopo Kata ya
Ndala, Manispaa ya Shinyanga.
Amesema kuwa kabla ya tukio hilo, marehemu alipokea
simu kutoka kwa mwanamke asiyejulikana aliyedaiwa kumueleza Pendo aachane naye,
jambo ambalo linadaiwa kuzua mabishano kati ya wawili hao.
Aidha, Kaimu Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwabundu, Kata ya
Ndala, amethibitisha kupokea taarifa za tukio hilo majira ya saa 12 asubuhi na
kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha
kuhifadhi maiti Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kwa uchunguzi zaidi,
huku mtuhumiwa akiendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano kabla ya
hatua za kisheria kuchukuliwa.
GUSA LINK HAPA CHINI👇
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment