" POLISI PWANI YAKAMATA WATU 10(WATATU WANAWAKE) KWA TUHUMA ZA KUPANGA UHALIFU

POLISI PWANI YAKAMATA WATU 10(WATATU WANAWAKE) KWA TUHUMA ZA KUPANGA UHALIFU











Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

Jeshi la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu kumi, wakiwemo wanawake watatu, wakidaiwa wakikusudia kukusanyika na kupanga njama za kufanya uhalifu.

Watuhumiwa hao wamekamatwa agost 16,2025 katika Ukumbi wa Mwitongo, uliopo Kata ya Mailimoja, Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.

Akithibitisha tukio hilo , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Salim Morcase, ameeleza taarifa za awali zilipatikana kupitia wasiri wa Jeshi hilo, zikieleza uwepo wa kundi hilo likihusishwa na mipango ya vitendo vya uhalifu.

Watuhumiwa waliokamatwa ni Focus Kasaka kutoka Mwanza, Harouna Zangina (Goba, Dar es Salaam), Abdallah Mazengo (Mwanana, Arusha), Samson Rabani (Tangini, Kibaha), Pendo Mwasomola (Nzovwe, Mbeya), Mkombozi Hatibu (Mailimoja, Kibaha), Mzambia Kabuje (Kijenge, Arusha), Furaha Mbise (Ubungo, Dar es Salaam), Upendo Msechu (KCMC, Moshi), na Upendo Mwalushwa (Mbezi, Dar es Salaam).

Uchunguzi wa kina unaendelea, na kwamba mara baada ya kukamilika kwa upelelezi, hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao.

Post a Comment

Previous Post Next Post