" Sherehe ya Utambulisho wa JEZI Mpya za Simba Kiingilio 250,000

Sherehe ya Utambulisho wa JEZI Mpya za Simba Kiingilio 250,000

 

Klabu ya Simba Sc imetangaza kuwa itazindua jezi mpya za Msimu za klabu hiyo Tarehe 27, 2025 katika Ukumbi wa Super Dome Masaki Jijini Dar es Salaam ambapo kiingilio cha kushiriki hafla hiyo kwa mtu yeyote atakayehitaji ni Tsh. Laki mbili na nusu kwa mtu mmoja Na yeyote atakayeshiriki kwenye uzinduzi huo atapata jezi zote tatu za msimu pamoja na vitu vingine vitakavyopatikana siku hiyo ndani ya ukumbi huo.

“Jezi za Simba msimu huu tutazindua kwa namna tofauti kidogo, ipo namna ambayo tumezoea jezi huwa zinazinduliwa lakini safari hii sababu tuna mdhamini mpya wa jezi kampuni ya JayRutty akishirikiana na kampuni ya kimataifa ya Diadora tukaamua kufanya kitu kipya chenye mvuto kwa jamii na biashara ya jezi kuwa na mvuto wa tofauti.”

“Jezi za Simba SC msimu wa 2025/26 zitazinduliwa tarehe 27/Agosti/2025, jezi zitazinduliwa majira ya saa 1:00 usiku na shughuli itafanyika kwenye ukumbi wa Super Dome uliopo Masaki. Safari hii tumefanya kuwa tukio lenye kubwa, tukio lenye hadhi ya ushua na kulifanya kuwa tukio bora ambalo litakutanisha wadau wakubwa wa Simba Sports Club na ambao wanataka kununua jezi ya Simba baada ya kuzinduliwa.”—Ahmed Ally akizungumza na waandishi wa habari siku ya leo.


Post a Comment

Previous Post Next Post