" Simba Watangaza Siku ya Kuadhimisha Simba Day 2025 …..

Simba Watangaza Siku ya Kuadhimisha Simba Day 2025 …..

 

Klabu ya Simba SC imethibitisha kuwa tamasha la kihistoria la Simba Day 2025 litafanyika tarehe 10 Septemba 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Klabu imesema siku hiyo itakuwa ni fursa kwa WanaSimba na Watanzania wote kusherehekea pamoja kupitia burudani mbalimbali zitakazopatikana kwenye sherehe hizo.

Taarifa ya klabu inaongeza kuwa sherehe ya Simba Day ni tukio la kila mwaka linalolenga kuunganishwa na mashabiki wake pamoja na kutoa burudani ya aina mbalimbali kwa jamii.


Post a Comment

Previous Post Next Post