" TAHAA YAMTANGAZA RAIS WAKE

TAHAA YAMTANGAZA RAIS WAKE

Na: Belnardo  Costantine(HA), Misalaba Media


 Chama cha kitaaluma cha wa Wasaidizi wa Afya Tanzania kimemtangaza mwanataaluma na mwanachama wa chama hicho   Bw.Timothy Cossan(HA ), kuwa Rais wa chama hicho kwa uapande wa Tanzania bara.

Bwana  Cossan(HA) amechaguliwa katika uchaguzi uliofanyika wakati wa kongamano la mkutano mkuu wa mwaka 2025 wa  chama hicho uliofanyika  mkoani Kilimanjaro katika ukumbi wa hospital ya KCMC  tarehe 28/9/2025

Sambamba na hilo uchaguzi  huo uliwakutanisha wanataluma na wajumbe  kutoka mikoa mbalimbali nchini, ikiwa sehemu ya kongamano la kitaaluma lililolenga kukumbushana wajibu wa kitaaluma na fursa zinazojitokeza kwa wasaidizi wa afya katika sekta ya afya nchini 

Hatahivyo mkutanao huo umeazimia kwa kura ya ndio ya maazimo ya kufanyika mkutano mkuu ujao  wa mwaka 2026 katika Jiji la dar es salaam,hili limetokana na wingi wa kura za wajumbe kuridhia mkutano kufanyika jijini dar es salaam.

Kwa upande wa hospital ya KCMC uliongozwa na  mkurugenzi wa hospital hiyo Professor  Masenga ambaye alikua mgeni rasmi katika kamano Hilo.

Katika hotuba yake amewaasa wanataluma na wanachama cha wasaidizi wa Afya Tanzania kuyaishi maadili ya kazi ili kuendeleza chachu ya maendeleo katika kutoa huduma za Afya nchini.

GUSA LINK HAPA CHINI👇


APPLICATION FORM

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

 

Post a Comment

Previous Post Next Post