Wachimbaji 25 katika Mgodi mdogo wa Madini ya dhahabu unaomilikiwa na kikundi cha Wachapa kazi Kijiji cha Mwongozo kata ya Mwenge mkoani Shinyanga wamefukiwa na kifusi baada ya mgodi huo kutitia wakati zoezi la ukarabati wa maduara ukiendelea.
Kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya ya Shinyanga ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro inaendelea na zoezi la uokozi kwa kushirikiana jeshi la zimamoto na uokoaji na wachimbaji katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa Mkuu wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro amesema jumla ya Wachimbaji 25 kutoka katika Maduara matatu tofauti wafukiwa na kifusi hicho katika duara namba 106,lilikuwa na Wachimbaji 6, na duara namba 103 wachimbaji 11 na duara namba 20 wachimbaji 8 na zoezi la uokoaji linaendelea.
Ajali hiyo imetokea Agosti 11,Mwaka huu wakati shughuli ya matengenezo maduara hayo ikiendelea ndipo ardhi ilititia na kuwafukia.
Post a Comment