" WANAFUNZI LAKI MBILI KUACHA SHULE KILA MWAKA

WANAFUNZI LAKI MBILI KUACHA SHULE KILA MWAKA

Na Lucas Raphael,TaboraNaibu katibu mkuu ofisi ya Raisi TAMISEMI upande wa elimu  Atupele Mwambene amesema kwamba wanafunzi zaidi ya 200,000 uacha shule kila mwaka kutokana na sababu nyingi zinachangiwa na walimu .Kauli hiyo ilitolewa jana wakati  akifunga mafunzo hayo kwa walimu wa awali na msingi zaidi ya 600 kutoka mikoa ya Simiyu, Katavi na Tabora yalifanyika katika chuo cha ualimu mkoani Tabora .Mwambene aliwataka walimu waliohudhuria mafunzo ya uendeshaji mpango wa shule salama kusimamia mienendo ya walimu wakorofi wanaosababisha ongezeko la wanafunzi wanaoacha shule.Alisema kwamba mpango wa serikali ni kuhakikisha  kila mwanafunzi anamaliza mzunguko wa elimu bila vikwazo vyoyote vya ndani na nje ya shule.Alisema kwamba vitu ambavyo vinachingia mdodoko wa wanafunzi  ni kutokana na  kusekana kwa  mazingira ya sio Rafiki ,viboko visivyokuwa na Idadi kwa wanafunzi ,vitisho na mengineo  Mwambene aliwataka walimu waliopata mafunzo hayo kupitia mpango wa shule salama kuakisha wanaondoa vikwazo hivyo kwa wanafunzi  wa elimu ya awali na msingi nchini.Alisema kwamba katika kipindi cha mwaka 2021/22 hadi 2024/25,   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Daktari  Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  aliwezesha upatikanaji wa ya shilingi zaidi trilioni 5.3 ambazo zilipelekwa  Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya utekelezaji wa afua  mbalimbali.Naibu katibu mkuu ofisi ya Raisi TAMISEMI alibainisha kwamba lengo ni  kuongeza uandikishaji na ubakizaji wa wanafunzi shuleni,  kuboresha ufundishaji na ujifunzaji, ujumuishi, usimamizi na uwajibikaji  katika elimu.Alisema kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 547.3 zimetokana na programu ya BOOST kwa ajili ya kuboresha miundombimu ya elimu awali na msingi .Mwambene alisema kwamba Miundombinu iliyojengwa na kukarabatiwa imewezesha kuongezeka kwa fursa kwa watoto wa rika lengwa  kuandikishwa na kuendelea na masomo bila kikwazo. Alisema hali iliyopelekea uandikishaji wa wanafunzi darasa la awali hadi kidato cha sita katika shule za Serikali kuongezeka kwa asilimia 14.98 kutoka  wanafunzi 14,359,406 mwaka 2021 hadi 16,510,972 mwaka 2024.Alisema kwamba uandikishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum  uliongezeka kutoka 28,482 mwaka 2020/21 hadi 78,429mwaka 2024.Alisema kwamba lengo la serikali n I kuhakikisha wanafunzi ananza elimu ya awali ,msingi hadi elimu ya lazima hakuna mtoto naweza kuacha shule .Awali mratibu wa mradi wa BOOST ofisi ya Raisi TAMISEMI Ally Swalehe aliwataka walimu hao kuhakikisha wanaifuta  miongozo yote ya Mpango wa Shule Salama  inatekelezwa kikamilifu katika shule mnazotoka.Alisema kwamba mnaporudi kwenye vituo vyenu vya kazi, muwajengee uwezo  kuhusu mpango wa shule salama walimu na wanafunzi wote waliopo shuleni kupitia mpango wa mafunzo endelevu ya walimu  kazini (MEWAKA). Mpango wa shule salama uliyopo chini ya mradi wa BOOST unaotekelezwa nchini, tayari umewafikia walimu 5061 kati ya walimu 5000 waliyolengwa kwa awamu hii ikiwa ni mafanikio yaliiyovuka malengo..Mwisho

 

Post a Comment

Previous Post Next Post