Na. Elias Gamaya- SHINYANGA
Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata jimbo la shinyanga mjini wameapichwa viapo viwili ikiwemo kiapo cha kujitoa uanachama wa chama chochote cha siasa pamoja na kiapo cha kutunza siri, mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mfawidhi wa wilaya ya shinyanga hakimu Agness Said Mlimbi leo tarehe Agosti 04, 2025.
Viapo hivyo vimefanyika katika ukumbi wa Mikutano chuo cha serikali za mitaa Mipango kampasi ya shinyanga ambapo Wasimamizi hao wamesisitizwa kufanya kazi chini ya misingi na utaratibu za tume huru ya taifa ya uchaguzi.
Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba 2025 ambapo Kaulimbiu ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025: ni “Kura Yako Haki Yako, Jitokeze Kupiga Kura"
Post a Comment