Na Mapuli Kitina Misalaba Juhudi za kuwaokoa wachimbaji 25 waliokuwa wamefunikwa na udongo katika machimbo ya Wachapa Kazi, Nyandolwa wilayani Shinyanga zinaendelea, ambapo hadi sasa watu saba wamepatikana.Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, kupitia taarifa yake ya jana Agosti 16, 2025, alisema awali watu watano waliokolewa, wawili kati yao wakifariki dunia na watatu wakiendelea vizuri, mmoja akipewa rufaa Bugando.Leo Agosti 17, wamepatikana wengine wawili wakiwa wamefariki dunia na kufahamika kwa majina ya Marco Ngelela na Macha Shaban, na hivyo idadi ya waliopoteza maisha kufikia watu wanne.Zoezi la uokoaji linaendelea kwa lengo la kuwapata wachimbaji wengine 18 ambao bado hawajafikiwa tangu ajali hiyo ya Agosti 11, 2025, ilipotokea wakati wa shughuli za ukarabati wa maduara.


Post a Comment