Benki Kuu ya Tanzania BOT imefanikiwa kukusanya hifadhi ya dhahabu ya Tani 9 ambayo nisawa na Shilingi Bilioni 1 tangu kuanzishwa kwa utaratibu wa kuhifadhi dhahabu katika benki hiyo
Hayo yamebainishwa na Rehema Kasimu, Afisa wa idara ya Masoko na fedha wa BOT wakati akizungumza na vyombo vya habari kwenye maonesho ya 8 ya kitaifa ya Teknolojia ya madini
- Geita baada ya Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa kutembelea banda ya BOT lililopo katika maonyesho hayo
Bi. Rehema amesema, BOT imeanzisha utaratibu huo wa kununua madini ya dhahabu ilikuongeza ifadhi ya fedha za nchi ambazo zitatumika kuimarisha uchumi wa nchi wakati wa mdororo wa kiuchumi
Aidha BOT pia imemzawadia Mhe Kassim Majaliwa Wallet yakutunza fedha za noto na fedha za sarafu ilikuendeleza utaratibu mzuri na sahihi wakuhifadhi fedha
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA





Post a Comment