HomeHABARI DKT. TULIA ACKSON AWAKABIDHI MILIONI 10 NA KOMBE LA UBINGWA ITEZI UNITED UYOLE MBEYA Misalaba Media September 06, 2025 0 Na Lydia Lugakila, Misalaba MediaMbeyaTimu ya Itezi United kutoka Kata ya Itezi mkoani Mbeya imetwaa ubingwa wa mashindano ya Tulia Trust Uyole Cup 2025 baada ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Timu ya chipukizi Fc ya Mkoani humo kwenye ligi iliyoshirikisha Idadi ya timu 35.Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa umoja wa mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson amekuwa mgeni rasmi katika mchezo huo na amewakabidhi mabingwa zawadi Itezi United shilingi milioni kumi pamoja na kombe la ubingwa huku akiahidi kuendelea kudhamini mashindano hayo Kwa miaka mitatu ijayo.Zawadi nyingine zilizotolewa ni mshindindi wa pili chipukizi Fc aliyepata zawadi ya shilingi milioni tano(5), mshindi wa tatu Airport Fc Waliopewa zawadi ya shilingi milioni tatu(3), pia zawadi Mmbalimbali zimetolewa Kwa wachezaji waliofanya vizuri kipa bora, mchezaji bora, mfungaji bora, timu yenye nidhamu, mwamuzi bora (Refa bora) na Kikundi bora cha ushangiliaji. 🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA You Might Like View all
Post a Comment