" DORMOHAMED ISSA AMUOMBEA MWALUNENGE NA DOKTA SAMIA KURA ZA KISHINDO MBEYA MJINI

DORMOHAMED ISSA AMUOMBEA MWALUNENGE NA DOKTA SAMIA KURA ZA KISHINDO MBEYA MJINI


Na Lydia Lugakila, Misalaba Media 

Mbeya

Mgombea wa udiwani kata ya Isanga kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dormohamed Issa, amewataka wananchi wa Jimbo la Mbeya mjini kuwa na imani na CCM na kumpa kura za kishindo Patrick Mwalunenge huku akiomba kura za kishindo kwa Dokta. Samia Suluhu Hassan mgombea Urais wa chama cha mapinduzi CCM.

Issa ametoa kauli hiyo katika uzinduzi wa kampeni za Jimbo la Mbeya Mjini zilizofanyika katika eneo la Kabwe Septemba 14, 2025.

 Akizungumzia Mwalunenge, mgombea udiwani huyo amesema kuwa Mwalunenge amekuwa msuluhishi wa migogoro mbalimbali, hivyo wana Mbeya Mjini wanakwenda kupata mtu sahihi.

Aidha, Issa amesisitiza kwamba Mwalunenge ni mtu shupavu na kwamba wana Mbeya Mjini wategemee kupata mafanikio, kwani ni mtu anayejali watu wote bila ubaguzi.

 Mgombea udiwani huyo alimuombea kura za kishindo Mwalunenge, pamoja na kwa Rais Dokta Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM wote huku akiwaomba Wana Mbeya mjini kutambua kazi kubwa zilizofanywa na Dokta Samia Suluhu Hassan na kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29,2025 kupiga kura.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post