" GOLD FM YASHEREHEKEA MIAKA MINNE YA MAFANIKIO

GOLD FM YASHEREHEKEA MIAKA MINNE YA MAFANIKIO

Kituo cha Redio Gold FM Tanzania kilichopo Manispaa ya Kahama, mkoa wa Shinyanga, leo Septemba 3, 2025, kimeadhimisha miaka minne tangu kuanzishwa kwake, safari iliyosheheni maudhui bora, burudani ya kipekee na vipindi vinavyogusa maisha ya jamii.

Kwa kipindi hicho, Gold FM imekuwa daraja la kuunganisha maelfu ya wasikilizaji kupitia muziki, taarifa za habari, michezo pamoja na vipindi mbalimbali vinavyobeba elimu na hamasa.

Kituo kimeendelea kukua na kujitanua kupitia masafa yake katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Shinyanga, Kahama, Mwanza, Geita, Tabora, Kagera, Simiyu, Mara na Kigoma.

Uongozi wa Gold FM umetoa shukrani kwa wasikilizaji, wadau na wadhamini wote kwa mchango wao mkubwa katika safari hii ya mafanikio, huku ukiahidi kuendelea kusikika na kutoa maudhui yenye ubora na mvuto zaidi.

Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu: #MinneYaDhahabu, yakionesha heshima na thamani ya safari ya pamoja kati ya kituo hicho na wasikilizaji wake.

🎙️ Gold FM – Sauti ya Dhahabu kutoka Kahama, inayogusa maisha kila siku.


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post