UJENZI wa majengo marefu kwenda juu unahitaji uimara kuanzia hatua ya msingi kwa kuwekewa kemikali zenye kuzuia unyevu nyevu kupita (waterproof) na hivyo kuleta nyufa zenye kusababisha madhara ya kuporomoka kwa nyumba.
Hayo yamebainishwa na wadau wa maendeleo katika maonesho ya Afrika Mashariki yaliyoanza Jijini Mwanza jana kwenye kibanda cha Tanzania Timeless Waterproof katika kiwanja cha Nyamagana kilicho katikati ya eneo hili ambalo ni kitovu kwa nchi za Ukanda wa Nchi za Maziwa Makuu.
Walisema kupatikana kwa malighafi ambazo zinasaidia kuzuia tofali, vigae na simenti kupenyeza maji ndani ni suluhisho kwa kudidimia kwa kwa majengo na hivyo kusababisha kuanguka chini hivyo kuleta madhara kwa binadamu.
Mkaazi wa mtaa wa Kapripoint ambaye ana ujenzi wa jengo la ghorofa, Maulid Juma alisema kuwa atanunua vifaa hivyo vyenye kuweza kuzuia maji kupenya kwani inafanya majengo kuwa imara zaidi.
Alisema uimara wa majengo ya ghorofa ni mhimu kuzingatiwa kwani madhara ambayo wanaweza kupata watu walio katika majengo hayo tatizo likitokea ni mkubwa na wenye athari kwa binadamu na vifaa.
Meneja mauzo wa Tanzania Timeline Waterproof, Sumilloh Iddi alisema wanazo waterproof membrane, Timeless App waterproof membrane, Timeless Self adhesive waterproof membrane, Timeless asphalt shingles na Timeless sawa tiles.
Alisema bidhaa hizo ni imara katika kuzuia kupenya kwa maji kwenda chini hivyo huimarisha nyumba na kuifanya kuwa imara kuhimili changamoto zinazojitokeza na kuathiri majengo.
Iddi aliwataka wakaazi wa Mwanza kununua hivyo katika kipindi hiki cha maonesho ya biashara ya Afrika Mashariki kwani wameweka punguzo kuwezesha watu wengi kumudu gharama yake.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment