HomeHABARI JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAIPONGEZA EMEDO KWA KUTOA MAFUNZO YA UOKOZI KWA WAVUVI WA BUSEKERA Misalaba Media September 26, 2025 0 Na Tonny Alphonce-Misalaba Media Watu 16 wa wilaya za Bunda,Musoma na Rorya wamepoteza maisha kutokana na kuzama katika ziwa Victoria Kwa mwaka 2024-2025Kutokana na ajali hizo za majini Kwa mwaka huo huo wa 2024-2025 watu 16 wamejeruhiwa baada ya kupata dhoruba ziwani.Akizungumza wakati wa utolewaji mafunzo ya Uokozi Kwa Wavuvi wa mwalo wa Busekera kaimu kamanda mkoa wa Mara Jeshi la Zimamoto na Uokoaji SSF Augustine Magere amesema sababu za vifo na majeruhi ziwa Victoria vinasababishwa na Upepo mkali,Wavuvi kubeba abiria na mizigo kupita kiasi,Baadhi ya wananchi kuongelea Ili Hali hawana ujuzi huo na baadhi ya Wavuvi na abiria kutovaa maboya wakiwa ziwaniSSF Magere amewataka wananchi wote na Wavuvi kuzingatia taarifa zinazotolewa na mamlaka ya Hali ya hewa Ili kujua Hali ya ziwani kabla ya kuingiaAidha SSF Magere amelipongeza Shirika la EMEDO Kwa kutoa mafunzo hayo ya Uokozi na kusaidia serikali kutoa elimu ambayo ilipaswa kutolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kwa upande wake Afisa Ufuatiliaji na Tathimini kutoka Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) Leonard Masele amesema kupitia Mradi wa Kuzuia Kuzama Maji Ziwa Victoria wanatarajia kutoa mafunzo ya Uokozi Kwa zaidi ya Wavuvi 100 wa mwalo wa Busekera."Tumeanza na awamu hii ya kwanza ambapo Wavuvi 15 wamepatiwa mafunzo ya namna ya kujiokoa wanapopata dhoruba ziwani,tulitoa mafunzo haya Mwanza na Sasa ni zamu ya Busekera mkoa wa Mara"alisema MaseleKwa upande wao Wavuvi waliopatiwa mafunzo hayo Moses Ouma na Jackson Magere wamelishukuru shirika la EMEDO na kuwataka kutoa elimu hiyo Kwa Wavuvi wengine Ili waweze kujiokoa pindi ajali inapotokea na kupunguza vifo vya majini.Shiriki la EMEDO linatekeleza mradi wa Kuzuia Kuzama Maji Ziwa Victoria unaofadhiriwa na Shirika la RNL la Uingereza,IRISH AID na ISLE OF Man Kaimu kamanda mkoa wa Mara Jeshi la Zimamoto na Uokoaji SSF Augustine Magere akizungumza.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA You Might Like View all
Post a Comment