Na Lydia Lugakila, Misalaba Media -Mbeya
Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (maarufu kama Kibajaji), amezungumza kuhusu umuhimu wa kumchagua Mwalunenge katika uchaguzi ujao wa Jimbo la Mbeya, akimtaja Mwalunenge kuwa ndiye msaada mkubwa katika maendeleo ya eneo hilo.
Lusinde ametoa kauli hiyo mnamo Septemba 14, 2025, katika uzinduzi wa kampeni za Jimbo la Mbeya mjini, ambapo amekumbusha wana Mbeya kuwa Mwalunenge alisaidia katika biashara yake alipokuwa nchini China hivyo moyo wake umejaa huduma kwa kila mtu.
Amehimiza umoja wa wapiga kura, akiwaasa wasiokuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumuunga mkono Mwalunenge ili kuleta mabadiliko katika Jimbo la Mbeya mjini.
Kibajaji amesisitiza umuhimu wa kumchagua Dkt. Samia kwa kura nyingi, huku akimtaka Mwalunenge kuwa kiongozi anayetetea maslahi ya vijana, hasa katika sekta ya usafiri wa bodaboda akieleza kuwa ni muhimu kuwalinda vijana dhidi ya unyanyasaji wa polisi wanapokamata pikipiki zao bila sababu za msingi.
Kibajaji alimaliza kwa kuwasihi viongozi na vijana kuishi kwa kuheshimiana na kuwapa kura za kutosha viongozi wa CCM ifikapo Oktoba 29, 2025.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment