Na Lydia Lugakila, Misalaba Media Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Karagwe kimezindua rasmi kampeni zake za uchaguzi katika viwanja vya Rwambaizi, Kata ya Kanoni, tukio lililohudhuriwa na mamia ya wanachama na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, tarehe 05 Septemba 2025.Mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (MNEC) wa CCM, Karim Amri, ambaye aliwahimiza wananchi kuendelea kuiamini CCM kutokana na rekodi yake ya uongozi thabiti na maendeleo endelevu.Kampeni hizo zimejikita katika kuwaomba wananchi kuichagua CCM na wagombea wa chama hicho akiwemo mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Ubunge wa jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa, pamoja na wagombea udiwani katika kata zote za wilaya hiyo.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment