
Wamiliki wa vyombo vya moto hususani pikipiki katika Manispaa ya Shinyanga wametakiwa kuacha kuwapa vyombo hivyo madereva wasio na sifa, ili kuepusha ajali zinazoweza kujitokeza.
Wito huo umetolewa na Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, wakati akitoa elimu kwa wamiliki wa vyombo vya moto ambapo amebainisha kuwa dereva asiye na sifa ni chanzo kikubwa cha ajali barabarani kutokana na kushindwa kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani.
Amesema dereva ambaye hajafuzu mara nyingi hukosa uelewa wa kutosha wa alama za barabarani, hawezi kufanya maamuzi sahihi na hivyo kuhatarisha maisha yake pamoja na watumiaji wengine wa barabara.
Aidha, Sajenti Ndimila amewatahadharisha wamiliki wa vyombo hivyo kuacha tabia ya kuwapa watoto pikipiki au vyombo vya moto vingine, kwa kuwa kutokana na umri wao hawawezi kumudu vyombo hivyo na mara nyingi hushindwa kufanya maamuzi sahihi wawapo barabarani, hali inayoongeza hatari ya ajali.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment