" JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA SHINYANGA MJINI YAAPA USHINDI MKUBWA KWA DKT. SAMIA NA WAGOMBEA WENGINE WA CCM

JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA SHINYANGA MJINI YAAPA USHINDI MKUBWA KWA DKT. SAMIA NA WAGOMBEA WENGINE WA CCM

Na Mapuli Kitina Misalaba 


Katibu wasaidizi wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Taifa, Antony Katala na John Maembe, leo Septemba 30, 2025, wamefanya ziara ya kampeni katika Wilaya ya Shinyanga Mjini ambapo wamekutana na viongozi pamoja na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo.

Katika ziara hiyo, viongozi hao wamepata nafasi ya kuzungumza na kusisitiza mikakati muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Wamewahimiza viongozi na wanachama kuendelea kusaka kura kwa wagombea wa CCM kuanzia ngazi ya taifa kwa mgombea urais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wagombea ubunge pamoja na madiwani wa chama hicho.

Aidha, wamehimiza Kamati ya Utekelezaji kufanya kazi kwa bidii, mchana na usiku, kuhakikisha CCM na wagombea wake wanapata kura nyingi za kishindo.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga, Regina Ndulu amesema jumuiya hiyo ya mkoa imejipanga kuhakikisha maagizo ya viongozi wa taifa yanatekelezwa kwa vitendo, huku akisisitiza mshikamano wa wanachama na viongozi wa ngazi zote ili kuongeza kura za wagombea wa CCM.

Akizungumza Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Kibabi, amewahakikishia viongozi hao kuwa jumuiya hiyo imejipanga kikamilifu huku akibainisha  kuwa wanatarajia kuanza kutembelea makundi mbalimbali ya wananchi ikiwemo kwenye masoko na minada ili kuwahamasisha kushiriki kikamilifu katika kupiga kura siku ya uchaguzi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mzee Fue Mrindoko, amesema jumuiya hiyo haitakubali kuona vitendo vinavyoweza kuharibu mchakato wa uchaguzi huku akiwataka wanachama kuendelea kushikamana na kuwa wamoja ili kuhakikisha ushindi wa chama hicho.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji akiwemo Bwana. Leonard Mapolu, amewahakikishia viongozi hao kuwa watayafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na kuendelea kutafuta kura kwa wagombea wa CCM.









 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post