JAMBO TANZANIA?
NAANDIKA KWA HERUFI KUBWA KUONESHA MSISITIZO...
HAWA MAFISADI WANAOJILIMBIKIZIA MALI WANAZONUNUA KUPITIA KODI ZETU WANANCHI NA KUSABABISHA UKOSEFU WA HUDUMA BORA ZA KIJAMII SIYO WATU WA KUWAFUMBIA MACHO NA KUWAKALIA KIMYA TENA....
HUDUMA BORA ZA KIJAMII SI KUWEPO KWA MAJENGO YA KUTOLEA HUDUMA HIZO BALI NI ZILE HUDUMA ZITOLEWAZO KWENYE MAJENGO HAYO....
SOTE NI MASHAHIDI WA BAJETI ZA WIZARA ZINAPOSOMWA NA KUPITISHWA, LAKINI HATUONI MABADILIKO YALIYOKUSUDIWA KWENYE HIYO BAJETI HUSIKA KWASABABU KUNA MABEPARI NA MAFISADI WANAJINEEMESHA WAO KWANZA HALAFU HUYU MTANZANIA ALIYEWEKEWA HIYO BAJETI BADO ANALIPIA HUDAMA NA ANAKOSA DAWA HOSPITALINI AKIPEWA MAELEKEZO YA KWENDA KUNUNUA DAWA DUKA LA JIRANI NA HAPO HOSPITALI...
MBALI NA HILO KUNA MTINDO WA KUMSHIKISHA MHUDUMU PESA MKONONI ILI UPATE HUDUMA YA HARAKA NA KUPEWA VIPAUMBELE, HII NI RUSHWA AMBAYO INACHELEWESHA HUDUMA KWA WASIO NA VIPATO KWASABABU BADO NCHI YETU HAINA USAWA WA VIPATO NA KUWAFANYA WAJIONE WANYONGE WASIO NA THAMANI, KITU AMBACHO KINALETA MANUNG'UNIKO NA KUONDOA IMANI NA AMANI YA MTU BINAFSI NA HATIMAYE KUKOSA IMANI NA SERIKALI, KUMBE KUNA UBOVU MAHALI WATU WANAPIGA WAPIGAVYO HATIMAYE WAAJIRIWA WA ENEO HUSIKA NA WAO PIA WANAKOSA HAKI ZAO ZA MSINGI IKIWEMO MARUPURUPU NA KUANZA KUTENGENEZA MAZINGIRA YA KUOMBA RUSHWA KWA WANAOHITAJI HUDUMA...
MIRADI INAKWAMAKWAMA NA KUPELEKEA KUCHUKUA MUDA MREFU KUMALIZIKA/KUKAMILIKA KWA DHANA AMBAZO BADO WANANCHI HAWAELEWI MPAKA SASA, KUMBE MAJAMAA YANAKULA TUU NA KUFANYA ANASA, HII NI DHULUMA....
MAFISADI NDIYO WANAOTUFELISHA HATA KWENYE MANUNUZI KWA AJILI YA KUHUDUMIA WANANCHI, WAO HUCHUKUA CHA KWAO KWANZA NA KUTUNUNULIA VITU VISIVYO NA UBORA NA KULITIA HASARA TAIFA LILILOWAAMINI KUWAPA MAJUKUMU YA KUSIMAMIA,
SI MMEJIONEA WENYEWE KWENYE MABASI YA MWENDOKASI AU NAONGOPA?
NAJUA MNAJUA MADUDU MENGI SANA, ILA NIPO HAPA KUWAHAKIKISHIA KUWA TUTAWASHUGHULIKIA HAO WANAOTUCHELEWESHA.
WATOTO WETU WA SHULE TULIZOAHIDIWA KUWA NI BURE NAKO NI MTITI KILA KUKICHA KUNA MCHANGO AMBAO HATA HAUELEWEKI, NI KWASABABU TU KUNA MAFISADI WACHACHE WASIO NA UCHUNGU NA MTANZANIA ANAYEIAMINI NA KUITUMAINIA SERIKALI NA KUSUBIRIA HUDUMA NA VILE TUNAVYOFATILIAGA BAJETI HALAFU UNAKUJA KUKUTANA NA VITU TOFAUTI HUKU CHINI......
CHAGUENI WENYEWE KINACHOFAA KWA MASLAHI MAPANA YA TAIFA LETU KWA AJILI YA VIZAZI VYETU.
SISI NCCR-MAGEUZI TUTAPAMBANA NA MAFISADI NA KUHAKIKISHA HAKUNA ANAYEIIBIA SERIKALI MAFUNGU YANAYOTOLEWA KWAAJILI YA KUBORESHA HUDUMA MUHIMU ZA KIJAMII PAMOJA NA MIUNDOMBINU..
Post a Comment