Na Lydia Lugakila - Mbeya
Mkuu wa mkoa wa Mbeya wakili Mhe, Beno Malisa amewaagiza maafisa wa Serikali wakiwemo afisa mazingira ardhi na mipango miji kuweka utaratibu mzuri wa utunzaji mazingira ikiwemo kutoruhusu mtu kujenga pasipo kupanda miti 20 katika eneo lake.
Mhe, Malisa ametoa kauli hiyo septemba 1, 2025 wakati akikabidhi pesa ya ruzuku kwa vikundi vya utunzaji wa mazingira katika mkutano maalum ulioandaliwa na shirika la Rikolto uliofanyika katika ukumbi Beaco jijini Mbeya.
Amesema kuwa jukumu la kutunza mazingira ni la kila mmoja na si vikundi wala Serikali bali kila mtu atakayetaka kuishi anahitaji kutunza mazingira.
Aidha kuhusu fedha hizo alizokabidhi mkuu huyo wa mkoa ameelekeza Rikolto na wanufaika kuhakikisha kuwa zinatunzwa katika shughuli husika na sio matumizi mengine.
Shukuru ni msimamizi wa mradi wa Rikoto amesema fedha hizo zitatumika kutunza mazingira kama kupanda miti ya matunda, miti ya kivuli pamoja na mboga za majani vile vile kutengeneza makorongo ya mto yaliyoharibiwa na mmomonyoko wa udongo.
Kikao hicho kimeudhuriwa na Halmashauri mbali mbali za ndani ya mkoa wa Mbeya ikiwemo Halmashauri ya wilaya ya Rungwe, Momba, Songwe, Busokelo pamoja na Halmashauri ya wilaya Mbeya.
Hata hivyo idadi ya vikundi vilivyokabidhiwa fedha kwa mkoa wa Mbeya ni vikundi 18 ambapo vimepewa shilingi milioni 40 na laki 2 na mkoa wa Songwe ni vikundi 10 ambapo vimepewa fedha kiasi cha shilingi milioni 22 na laki 5.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment