" SHANGWE ILIVYOTAWALA WANANCHI NA VIONGOZI WAKIMUOMBEA KURA ZA KISHINDO MGOMBEA UDIWANI KATA YA NSALAGA JIMBO LA UYOLE

SHANGWE ILIVYOTAWALA WANANCHI NA VIONGOZI WAKIMUOMBEA KURA ZA KISHINDO MGOMBEA UDIWANI KATA YA NSALAGA JIMBO LA UYOLE

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media

Mbeya

Ilikuwa shagwe na vigelegele kwa wananchi wa kata ya Nsalaga Jimbo la Uyole mkoani Mbeya waliofika katika eneo la kata hiyo kushuhudia uzinduzi wa kampeini za CCM katani humo zilizofanyika Septemba 17,2025 .

Wananchi hao walifika kumsikiliza mgombea udiwani wa kata ya Nsalaga Clemence James Mwandemba kijana mdogo kuliko wote aliyeonekana kuwavutia walio wengi.

Zoezi lililotangulia mkutano huo lilikuwa ni kuwaombea kura za heshima na za kishindo viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) akiwemo mgombea nafasi ya Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan  mgombea ubunge Jimbo la Uyole Dokta Tulia Ackson na mgombea udiwani kata Nsalaga Clemence Mwandemba.

Awali akipanda jukwaa hilo mjumbe Halmashauri kuu ya wilaya Rodrick Leonard Mwaiteleke aliyeongoza zoezi hilo alimpongeza mgombea huyo wa udiwani kutokana na harakati zake ambazo amekuwa akizifanya akiwa hajagombea nafasi hiyo.

"Bado Mwandemba hajashika wadhifa huo wa udiwani huo lakini tayari ameisha omba Barabara za kata ya Nsalaga kupitia vikao vikuu.

"Nawashukuru wajumbe walifanya jambo jema kutuletea kijana Mwandemba (dogo Janja) kwani  Halmashauri ya Jiji la Mbeya inakwenda kuwa diwani mdogo  hakika wamechagua maendeleo" alisema Mwaiteleke.

Amesema spidi ya awali ya Clemence Mwandemba  ilimshangaza sana kwani alifanya kazi kwa viendo huku akiwaomba wananchi hao kujitokeze kwa wingi oktoba 29, 2025 kuwapigia kura Dkt. Samia Suluhu Hassan Dkt.Tulia na mgombea udiwani huyo.

Naye katibu wa Taasisi ya Mtetezi wa Mama Mkoa wa Mbeya Boazi Mwasongole amesema kuwa Mwandemba amekuwa Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) Mbeya mjini hakuweza kuwaacha vijana wa kata ya Nsalaga kwa Fursa mbali mbali za kiuchumi huku akiwaomba kuweka kura nyingi kwa Dokta Tulia kutokana na kuliheshimisha Taifa kwa uongozi imara.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Madreva bajaji Uyole  Joseph Kayala amesema kuwa Mwandemba amekuwa kijana wa mfano kwani aliwahi wasaidia sana hasa katika ukarabati wa Barabara zilizoonyesha kuwakwamisha wananchi katika shughuli za maendeleo na kumtaja mgombea huyo kuwa ni msikivu kwa kila mtu.

"Sisi madreva bajaji alitusaidia kipindi cha mvua leo ameomba Barabara za Nsalaga ni jambo jema kwetu kwani Nsalaga tunahitaji kupata mtu sahihi Kama huyu"alisema Kayala.

Naye Mgombea udiwani kata ya Mwasanga Brandy Nelson Mwinuka amesema kuwa kila mtu anajua ni jinsi gani chama cha mapinduzi(CCM) kimefanya kazi kubwa hivyo wakichague kwa kishindo ili kiwaletee maendeleo.

"Nsalanga mmepata jembe maana Mwandemba ni kijana ambaye anaweza kupitia sehemu hata zisizopitika hivyo tumchague ili aibadili kata yetu"alisema Mwinuka.

Aidha Katibu ya vijana wilaya ya Mbeya mjini Raphael Mollel amesema wana Nsalaga wamepata mtu sahihi hivyo wajipange kumpa kura nyingi atawale hadi kichwa kiote mvi huku akimuomba mgombea huyo kuwatetea wananchi hasa wanyonge.

Hata hivyo naye mgombea udiwani kata ya majengo Maulid Khamis amesema viongozi hao wamejidhatiti kuwaletea maendeleo wananchi hao hivyo wasiwe na wasisi na viongozi hao kwani changamoto zao zote zitatatuliwa


 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post