Na Mapuli Kitina Misalaba
SERIKALI imeeleza kuwa uwekezaji wa viwanda, hususan
vinavyoongeza thamani ya mazao ya kilimo na mifugo, ni nguzo muhimu ya kukuza
uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla, huku ikitoa pongezi kwa Jambo Group of
Companies kwa mchango wake mkubwa katika ajira, ulipaji kodi na maendeleo ya
sekta ya maziwa.
Kauli hiyo imetolewa leo Januari 9, 2026 mkoani Shinyanga
wakati wa ziara ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi pamoja na Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, waliotembelea kiwanda cha Jambo Group
kinachojihusisha na uchakataji wa maziwa na bidhaa za matumizi ya kila siku
(FMCG).
Akisoma taarifa fupi ya kampuni hiyo, Mkurugenzi wa Jambo Group Khamis Salum ameeleza kuwa
Jambo ni kiwanda cha Kitanzania kilichoanzishwa kwa dhamira ya kuwa mfano kwa
wawekezaji wengine wazawa, akisisitiza kuwa Watanzania wana uwezo mkubwa wa
kujenga viwanda vikubwa na endelevu.
Katika upande wa ajira, ameeleza kuwa Jambo Group
inaajiri wafanyakazi zaidi ya 1,000 wa kudumu, huku ajira za muda na zisizo za
moja kwa moja zikifikia zaidi ya watu 10,000, hali inayochangia kwa kiasi
kikubwa kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira, hasa kwa vijana na wanawake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jambo Group Mhe. Salum Khamis
Mbuzi ameeleza kuwa mradi wa maziwa unaotekelezwa na Jambo Group una thamani ya
dola za Marekani milioni 45, huku thamani ya jumla ya kiwanda hicho kwa sasa
ikifikia takribani shilingi trilioni 1.2. Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, miradi
hiyo inalenga kujenga uchumi wa wananchi na kuchangia moja kwa moja kwenye
mapato ya Serikali.
Ameongeza kuwa Jambo Group imeamua kuwa mzalendo kwa
kulipa kodi kwa uwazi na uaminifu, ambapo kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), kampuni hiyo kwa sasa inachangia takribani shilingi
bilioni 12 kwa mwezi na kwamba kampuni imeendelea kuwa miongoni mwa walipa kodi
wakubwa hususan katika Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza katika ziara hiyo, Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Pius Stephen Chaya, ameeleza
kuwa mwelekeo wa Serikali kwa sasa umejikita zaidi kwenye uwekezaji, kwa lengo
la kuwapatia wakulima na wafugaji masoko ya uhakika ya mazao yao.
Amesema kuwa Tanzania ina wakulima na wafugaji wengi,
lakini changamoto kubwa imekuwa ni kukosekana kwa maeneo ya kupeleka mazao ili
yaweze kuongeza thamani na kuleta faida halisi kwa wananchi ambapo kwa msingi
huo, anasema Serikali inahitaji wawekezaji kama Jambo Group wanaoamua kuwekeza
kwenye viwanda vinavyowagusa wananchi moja kwa moja.
Naibu Waziri huyo ameipongeza kampuni ya Jambo Group
kwa mchango wake katika ajira, akieleza kuwa kuajiri wafanyakazi zaidi ya 1,000
wa kudumu na takribani 10,000 wa muda ni mchango mkubwa kwa Taifa huku akiongeza
kuwa ili uchumi wa nchi uendelee kukua, ni lazima Serikali na sekta binafsi
ziwekeze zaidi kwenye viwanda, hususan vya watu binafsi na mashirika ya umma.
Ametoa wito kwa wawekezaji wengine kuiga mfano wa
Jambo Group, akisisitiza kuwa ni mwekezaji wa Kitanzania aliyeamua kujitoa
kusaidia jamii na kwamba Serikali itaendelea kutoa ushirikiano na kuunga mkono
jitihada za uwekezaji wa kampuni hiyo ili kuhakikisha kiwanda kinaendelea kukua
na kuongeza ajira kwa manufaa ya wakulima na wafugaji, hususan wa Kanda ya
Ziwa.
Kwa upande wake, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Balozi Dkt.
Bashiru Ally Kakurwa amefikisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akieleza kuwa Serikali ya Awamu ya
Sita iko tayari kutekeleza yote yaliyoahidiwa kupitia Ilani ya Chama Cha
Mapinduzi huku akiwaomba wananchi na wadau wa maendeleo kuendelea kutoa
ushirikiano kwa Serikali na kumuombea Rais ili aendelee kuliongoza Taifa kwa
hekima na mafanikio.
Waziri huyo amesema kuwa ameridhishwa na hatua zote za
maendeleo alizoziona katika kiwanda cha Jambo Group, akisisitiza kuwa milango
ya Serikali iko wazi kutoa huduma na kuwezesha wawekezaji katika sekta zote.
Anafafanua kuwa changamoto zitakazoshindikana kutatuliwa katika ngazi ya wizara
zitapelekwa kwa Waziri Mkuu, na endapo zitahitaji maamuzi ya juu zaidi,
zitafikishwa kwa Makamu wa Rais na hatimaye kwa Rais.
Anaeleza kuwa dhamira ya Serikali ni kuweka mazingira
salama na rafiki kwa wafugaji, wavuvi, wakulima, wafanyabiashara na wawekezaji,
ili Tanzania iweze kujenga uchumi imara, shindani na unaojitegemea.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, ameeleza
kuwa uwepo wa Jambo Group Mkoani Shinyanga ni fahari kubwa kwa Mkoa na ni
ushahidi wa vitendo kuwa Shinyanga ni eneo salama na rafiki kwa uwekezaji.
Ameeleza kuwa miradi mikubwa kama hiyo imekuwa
kichocheo cha maendeleo ya wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kwa kuongeza ajira,
kipato cha kaya na mzunguko wa fedha katika maeneo ya vijijini na mijini.
Mhe. Mhita amesema Serikali ya Mkoa itaendelea
kushirikiana kwa karibu na wawekezaji wote wanaokuja Shinyanga, kwa kuhakikisha
mazingira ya biashara na uwekezaji yanabaki kuwa tulivu, salama na yenye
ushirikiano, ili Mkoa uendelee kuchangia kikamilifu katika uchumi wa Taifa.


Mkurugenzi Mtendaji wa Jambo
Group Mhe. Salum Khamis Mbuzi akieleza mchango wa kiwanda hicho katika
ajira, ulipaji kodi na maendeleo ya sekta ya maziwa leo wakati wa ziara ya
viongozi wa Serikali mkoani Shinyanga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jambo
Group Mhe. Salum Khamis Mbuzi akieleza mchango wa kiwanda hicho katika
ajira, ulipaji kodi na maendeleo ya sekta ya maziwa leo wakati wa ziara ya
viongozi wa Serikali mkoani Shinyanga.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Balozi
Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akizungumza wakati wa ziara ya kikazi kiwandani hapo,
akieleza dhamira ya Serikali ya awamu ya sita katika kuweka mazingira rafiki
kwa wawekezaji.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Pius Stephen Chaya akisisitiza
umuhimu wa uwekezaji wa viwanda katika kuwasaidia wakulima na wafugaji kupata masoko
ya uhakika.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe.
Mboni Mhita akizungumza
kuhusu umuhimu wa uwekezaji wa Jambo Group katika kukuza uchumi wa Mkoa wa
Shinyanga.

Mkurugenzi wa
Jambo Group Khamis Salum, akisoma taarifa fupi ya kampuni hiyo leo Ijumaa
Januari 9, 2026 wakati wa ziara ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi pamoja na Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji katika kiwanda hicho.

Ziara ya Waziri na Naibu Waziri katika kiwanda cha Jambo Group ikilenga kujionea uwekezaji wa kisasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jambo Group Mhe. Salum Khamis
Mbuzi akiwaongoza viongozi wa Serikali na Mkoa wa Shinyanga kutembelea sehemu
mbalimbali za kiwanda hicho na kuwaeleza hatua za uzalishaji na uwekezaji
uliofanyika.

Viongozi wa Serikali wakitembelea miundombinu ya uchakataji wa katika kiwanda cha Jambo Group mkoani Shinyanga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jambo Group Mhe. Salum Khamis
Mbuzi akiwaeleza hatua za uzalishaji na uwekezaji
uliofanyika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jambo Group Mhe. Salum Khamis
Mbuzi akiwaeleza hatua za uzalishaji na uwekezaji
uliofanyika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jambo Group Mhe. Salum Khamis
Mbuzi akieleza hatua za uzalishaji na uwekezaji
uliofanyika.
Viongozi wa Serikali wakijionea mitambo ya kisasa ya uchakataji wa maziwa iliyowekezwa na Jambo Group.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jambo Group Mhe. Salum Khamis Mbuzi akieleza hatua za uzalishaji na uwekezaji uliofanyika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jambo Group Mhe. Salum Khamis Mbuzi akieleza hatua za uzalishaji na uwekezaji uliofanyika.
Viongozi wa Serikali wakijionea mitambo ya kisasa ya uchakataji wa Juice ya Maembe iliyowekezwa na Jambo Group.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jambo Group Mhe. Salum Khamis Mbuzi akieleza hatua za uzalishaji na uwekezaji uliofanyika.
Ziara ya Waziri na Naibu Waziri katika kiwanda cha Jambo Group ikilenga kujionea uwekezaji wa kisasa.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


























Post a Comment