Jumuiya ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii
Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga inawaalika wananchi wote wa mkoa huo
kushiriki katika zoezi la kuchangia damu salama kwa lengo la kuokoa maisha ya
watu wenye uhitaji.
Akizungumza Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga
Nabila Kisendi amesema kampeni hiyo inalenga kuhamasisha mshikamano wa kijamii
kwa kuhakikisha hospitali zinakuwa na hifadhi ya damu ya kutosha kwa ajili ya
wahitaji.
Sambamba na kuchangia damu, wananchi watakaohudhuria
watapata pia huduma za bure za kupima afya ikiwemo shinikizo la damu
(pressure), kiwango cha sukari mwilini pamoja na magonjwa mengine ya hali ya
maisha.
Huduma hizi zitatolewa kwa ushirikiano wa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kupitia ofisi ya Mganga Mfawidhi wa Mkoa.
SMAUJATA imewaomba wadau na wananchi kujitokeza kwa
wingi kushiriki katika zoezi hilo, kwani kila tone la damu linalotolewa lina
mchango mkubwa katika kuokoa maisha ya wagonjwa, hususan wajawazito, watoto, na
wahanga wa ajali.
Zoezi la kuchangia damu linatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi wiki hii katika eneo la stand ya Hiace karibu na soko kuu la Mkoa wa Shinyanga

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment