" WANA IGURWA MCHAGUENI FABIUS CLAVERY KWA MAENDELEO KABAMBE

WANA IGURWA MCHAGUENI FABIUS CLAVERY KWA MAENDELEO KABAMBE

 Na Lydia Lugakila 

Mgombea udiwani kata ya Igurwa iliyopo wilayani Karagwe mkoani Kagera kupitia chama cha ACT Wazalendo Fabius Boniventure Clavery ameahidi kukamilisha miradi yote iliyokwama katani humo ikiwemo Ile iliyoanzishwa kwa nguvu ya wananchi, endapo atapewa ridhaa ya kuwa diwani wa kata hiyo.

Akizungumza na vyombo vya habari Fabius amesema kuna miradi ikiwemo Zahanati, shule za msingi,miradi ya maji na umeme ambayo imekwama kwa muda mrefu sasa hivyo kata hiyo inahitaji mtu mwenye weledi wa kuisemea na kuwasemea wananchi ili ikamilishwe na ianze kutoa huduma kwa wananchi.

Aidha mgombea huyo amewaahidi wananchi wa kata hiyo kila kitongoji kupata umeme ili kukuza uchimi wa mwananchi mmoja mmoja kupitia shughuli za kibiashara.

Kuhusu miundombinu ya barabara, Fabius ameahidi kutengenezwa kwa barabara za kata hiyo ikiwemo ya Omukigando-Igurwa ambayo imekuwa korofi hivyo kurudisha nyuma shughuli za usafiri na safirishaji katika kata hiyo, pamoja na kupunguza mlima katika eneo la Omkisanje ambao umekuwa ukisababisha ajali nyingi.

Pia mgombea huyo kupitia ACT Wazalendo amewaahidi vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kuwatafutia fursa mbalimbali ikiwemo mikopo, lakini pia kuhakikisha mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na halmashauri inawafikia walengwa bila ubaguzi.

Sanjali na hayo amewaahidi wananchi wa kata ya Igurwa utatuzi wa migogoro ya ardhi ambayo ipo katika kata hiyo ila kutunza Amani na utulivu wa Igurwa, ikiwa ni pamoja na kutumika zaidi kama mwakilishi wa wananchi kuliko kutumikiwa

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post