" AMUUA MAMA YAKE WA KAMBO KISA MALI ZA URITHI

Top News

AMUUA MAMA YAKE WA KAMBO KISA MALI ZA URITHI

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media

Mbeya

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja aitwaye Matatizo Yohana mkazi wa masoko  Mkoani Mbeya  kwa tuhuma za mauaji  ya Mama yake  wa kambo aitwaye Merry Yohana (61) aliyekuwa mkazi wa masoko kwa kumkata na panga kichwani.

Akitoa taarifa hiyo kamanda  wa jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Benjamini Kusaga amesema mtuhumiwa huyo alitenda tukio  hilo mnamo Oktoba 06,2025 majira ya saa 2 kamili asubuhi katika kijiji cha mapinduzi kata ya masoko tarafa ya Isanga mkoani Mbeya kwa kumuua Bi Merry  Yohana ambaye pia alikuwa mkazi wa masoko mwenye uhalbino.

"Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya lilianza msako mkali na kufanikiwa  kumkamata mtuhumiwa huyo majira ya usiku katika kijiji cha mapinduzi kata ya masoko kuhusiana na tukio hilo kuzaga na kueleza chanzo cha tukio hilo" alisema kamanda huyo.

Uchunguzi wa awali wa tukio hilo umetajwa kuwa ni mgogoro wa kifamilia kuhusu mashamba ambapo mtuhumiwa alikuwa akimshinikiza mtuhumiwa Bi Merry Yohana ambaye kwa sasa ni marehemu kugawa mashamba ya urithi ambayo yaliachwa na Baba yake mzazi aliyefariki alisema Acp kuzaga"

Hata hivyo Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa baadhi ya vijana kuhusu tamaa ya kutaka kujipatia mali kwa njia zilizo kinyume na sheria uchunguzi unakamilishwa ili hatua nyinginezo zichukuliwe dhidi ya mtuhumiwa kwa mujibu wa sheria.

Post a Comment

Previous Post Next Post