Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa
kuwasili mkoani Shinyanga siku ya Jumamosi, Oktoba 11, 2025, kwa ajili ya
kufanya mikutano ya kampeni.
Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, Rais Samia
ataianza kwa kuwasalimia na kuomba kura kwa wananchi wa Wilaya ya Kishapu kabla
ya kufanya mkutano wa hadhara utakaofanyika kuanzia saa nne asubuhi katika
Uwanja wa CCM Kambarage, mjini Shinyanga.
Baada ya mkutano huo, Dkt. Samia ataendelea na ziara
yake mkoani humo ambapo anatarajiwa kufanya mkutano mwingine wa hadhara kuanzia
saa nane mchana katika Uwanja wa Magufuli, Manispaa ya Kahama.
Akizungumza na Misalaba Media, Katibu wa Siasa, Uenezi na
Mafunzo wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Bwana Richard Raphael Masele, amethibitisha
taarifa hizo na kuwakaribisha wananchi wote kujitokeza kwa wingi kushiriki
katika mikutano hiyo ya kampeni.
Masele amehimiza wananchi wa Shinyanga kutumia fursa
hiyo kumsikiliza mgombea huyo wa CCM akieleza sera na ahadi zinazolenga kuleta
maendeleo endelevu kwa Watanzania wote.

Post a Comment