Peter A. Frank Lugumi (Mr. Black) mkurugenzi wa The BSL Investment Company Limited na BSL SCHOOLS TANZANIA na RWANDA ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi kwenda vijana (CCM Shinyanga mjini) Leo ameendelea na ziara yake nchini Rwanda baada ya kutoka Ikulu ya Uganda hapo jana tarehe 8/10/2025 na leo tarehe 9/10/2025 amepata wasaha wa kutembelea Bunge Tukufu la Rwanda kwa ajili ya kuendeleza mahusiano na kuitangaza zaidi nchi ya Tanzania kidiplomasia. Mr. Black pia amepata wasaha wakupokelewa katika ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda kwa ajili ya kutambulisha shughuli zilizompeleka nchini humo. Alipata wasaha wa mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Balozi Dr. Habib Gallus Kambanga pia afisa uwekezaji katika ubalozi Ndugu Mosses E. Mosses. Ziara hii imezaa matunda mengi mara baada pia ya kukutana na bodi ya uwekezaji ya Rwanda (RDB). Mr. Black pia amepata nafasi ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria nchini Rwanda katika kukuza na kuendeleza historia ya Afrika Mashariki pia utalii ndani ya jumuiya hii. Kupitia muendelezo wa ziara hii Mr. Black anaendelea kuwahamasisha vijana wote wa Tanzania na Afrika Mashiriki kiujumla kulinda amali na historia njema ya mataifa yetu pasina kuchafua amani na kuendeleza mshikamano zaidi.
Mr. Black akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda katika ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda
Mr. Black akiingia katika Bunge Tukufu la Rwanda kwa shughuli maalumu

Post a Comment