Na Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha. Akizungumza katika maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi Jijini Arusha Afisa Tarafa Themi Chausiku Quamo amewataka watoto wa kike kuepuka vishawishi vinavyoweza kupelekea kukatiza ndoto zao, na kupongeza idadi kubwa ya watu wazima wanaoendelea kujitokeza kupata elimu hiyoAmetoa rai hiyo na kuwataka kuongeza bidii katika masomo yao baada ya kupewa nafasi ya pili ya kurudi shule, ili waweze kutimiza malengo yao.Sambamba na hayo ametoa wito kwa jamii kuchangamkia fulsa ya kusoma elimu ya watu wazima ili kupata maarifa na ujuzi. "Nawakumbusha kuendelea kudumisha amani na utulivu katika kipindi hiki tunapojiandaa na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu" amesema Chausiku. Katika kipindi hiki ambacho serikali ina mpango wa kila shule kuhakikisha inatoa mafunzo ya elimu ya amali, kituo cha elimu ya watu wazima cha MUKEJA kilichopo shule ya msingi Levolosi Jijini Arusha kimewanoa watu wazima zaidi ya miatatu tangu kuanzishwa kwake 2013, kinatoa mafunzo ya ufundi wa ushonaji, ususi, kupika na ujasiliamali. Kwa upande wake Afisa elimu watu wazima Mkoa wa Arusha Emmanuel Mahundo amesema lengo la mpango huo ni kuona kila mmoja ananufaika na elimu hiyo, amemshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwezesha ujenzi wa shule 27 za sekondari katika mkoa wa Arusha, wasichana takriban 244 wamenufaika na mpango wa elimu SEQUIP kwa vituo 12 mkoa mzima, lengo likiwa ni kusukuma mbele sekta ya elimu. Vile vile Mkufunzi Mkazi elimu ya watu wazima mkoa wa Arusha Aminiel Vavayo mesema kupitia mradi wa SEQUIP umewasaidia watoto wa kike zaidi ya mia tatu waliokatisha masomo yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mimba, hali duni na ukatili, wamenufaika na sasa wanaendelea na masomo. "Katika mkoa wetu tumepiga hatua kutokana na uwepo vituo vya kutosha vya elimu ya watu wazima, elimu ambayo kila mhitaji anaweza kuipata wakati huo akiendelea kufanya shughuli zake nyingine"amesema Vavayo. Kwa upande wake Mwalimu wa kituo cha Mpango wa Uwiano Kati ya Elimu na Jamii (MUKEJA) Amina Bakari amesema katika utoaji wa elimu ya kwa watu wazima anakumbana na changamoto za utoro kwa wananfunzi wake, hatua inayombidi kuwapa zawadi kama motisha ili kuwavutia wanafunzi wake kuhudhuria masomo. "Najivunia kuona wanafunzi wangu wanapata maarifa na kujipambanua, natoa wito kwa jamii kujiunga na elimu ya watu wazima inayotolewa bila malipo" amesema Mwl.Amina.Kwa upande wake mnufaika wa mafunzo ya elimu ya watu wazima Oliva Shayo (46) ameshukuru na anajivunia kuondokana na utegemezi baada ya kupata ujuzi wa kushona nguo."Nilijiunga na masomo mwaka 2017 nikiwa na watoto (5), kwa kuwa nilikuwa na nia nilipata ujuzi na sasa nimefanikiwa kununua mashamba na ninajipatia kipato cha kutosha kupitia fani ya ushonaji, nawashauri wanawake wenzangu kuacha woga, waje hapa waondoe ujinga, wapate maarifa ili kusukuma gurudumu la maisha" Amesema Oliva. Pia Songo Meere ameshukuru hatua aliyofikia ya kujua kusoma na kuandika katika kituo cha MUKEJA na kuahidi kuendelea kuwahamasisha vijana wengi jamii ya Kimasai ambao hawajui kusoma na kuandika ili waweze unufaika na fulsa hiyo. "Nilikuja mjini kufanya shughuli za ulinzi lakini kwa bahati nzuri nilifanikiwa kupata fulsa ya kusoma na sasa ninaweza kusoma, kuandika na kuhesabu. Nitaendelea na masomo hadi elimu ya juu" amesema Songo. Zamzam Madame mhitimu wa kidato cha nne amepata ujuzi wa kushona, kupika, kutengeneza lishe ya watoto na watu wazima"Naamini kuwa kufeli shule sio kufeli maisha, matarajio yangu ni kufanya shughuli zaidi ya moja ili kuharakisha maendeleo yangu na kujikwamua kiuchumi" amebainisha.

_Mgeni rasmi Afisa Tarafa Themi Chausiku Quamo (aliyevaa suti) akikagua kazi za wanafunzi wa elimu ya watu wazima katika shule ya msingi Levolosi Jijini Arusha_

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment