Madereva wa vyombo vya moto katika Mkoa wa Shinyanga wamepewa elimu ya kuzingatia na kutii sheria za usalama barabarani kwa kuhakikisha wanaweka namba sahihi za usajili kwenye vyombo vyao kabla ya kuvitumia barabarani.
Akitoe elimu hiyo, Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, amewataka kutekeleza matakwa ya kisheria bila shuruti kwa kuepuka kuendesha vyombo vya moto visivyo na namba za usajili au vyenye namba zisizokamilika.
Amesema kuweka namba za usajili sahihi kunarahisisha utambuzi wa chombo husika na kumsaidia dereva kuepuka mkono wa sheria, huku pia kikiwa ni hatua ya kulinda usalama wa watumiaji wengine wa barabara.
Sajenti Ndimila ameongeza kuwa baadhi ya madereva wamekuwa wakihusishwa na makosa ya jinai ikiwemo ajali au uhalifu, lakini hukosa kufahamika haraka kutokana na vyombo vyao kutokuwa na namba za usajili zinazotambulika, jambo ambalo ni hatari kwa jamii.
Aidha, amewataka madereva hao kujijengea tabia ya kutii sheria bila kulazimishwa, kwa kuwa kufanya hivyo kutawasaidia kuepuka usumbufu na kulinda maisha yao pamoja na ya watumiaji wengine wa barabara.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA






Post a Comment