" WADAU WA TUMBAKU WASIOSHIRIKI ZOEZI LA USAJILI WA WAKULIMA KUFUNGIWA KUFANYA KAZI – WAZIRI BASHE

WADAU WA TUMBAKU WASIOSHIRIKI ZOEZI LA USAJILI WA WAKULIMA KUFUNGIWA KUFANYA KAZI – WAZIRI BASHE

Na Lucas Raphael, Misalaba Media -TaboraWaziri wa Kilimo,Hussein Bashe, amesema wadau wa zao la tumbaku nchini ambao hawatashiriki katika zoezi la usajili wa wakulima wa tumbaku hawataruhusiwa kufanya kazi na wakulima, ikiwemo vyama vya ushirika nchini.Alitoa kauli hiyo jana mkoani Tabora, wakati wa kikao kazi kilicholenga kuboresha huduma ya bima ya mazao na kuhakikisha mkulima analindwa dhidi ya majanga yanayoweza kuathiri uzalishaji. Alisema kuwa, bima kwa wakulima ni jambo la lazima kwa sasa, kwani inalenga kuwalinda wanapokumbwa na majanga kama ukame, magonjwa au majanga mengine ya asili. Alibainisha kuwa, Serikali ina muelekeo mahsusi wa kuhakikisha kila mkulima nchini anakuwa na bima ya mazao ili kujenga misingi ya kilimo biashara chenye tija.“Ni lazima tuweke mazingira mazuri kwa wakulima kufanya kilimo biashara. Tunataka kila mkulima wa tumbaku awe amesajiliwa na awe na bima ya mazao yake,” alisema Bashe.Aidha Bashe alielekeza  kuanzishwa kwa bima ya ushirika ambayo itasimamiwa na benki ya Ushirika na ambayo itakuwa inamlinda mkulima kuanzia mwanzo anapoandaa shamba mpaka wakati wa mavuno ya tumbaku yake"Kwa pamoja tumekubaliana  wakulima wa zao hilo Tabora  wawe wamefanyiwa  usajili wa mashamba yao na Wapate  bima ya zao hilo kwani jukumu la Serikali ni kumlinda Mkulima" alisema BasheBashe aliongeza kuwa kufikia Oktoba 30 mwaka huu, kampuni za ununuzi wa tumbaku ambazo hazitakuwa zimelipa madeni yao kwa wakulima hazitaruhusiwa kupewa leseni ya kununua tumbaku katika mkoa wa Tabora.Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, amemshukuru Waziri wa Kilimo kwa hatua anazochukua kulinda maslahi ya wakulima, huku akisisitiza haja ya kufanyiwa mapitio upya kwa mfumo wa sasa wa bima ya tumbaku, kutokana na mapungufu yaliyopo ambayo yamekuwa yakiwaathiri wakulima.Alisema, kuna umuhimu wa kuwepo mkakati wa kitaifa wa kuwalinda wakulima dhidi ya hasara.Mwisho


 

Post a Comment

Previous Post Next Post