HomeHABARI WIZARA YA MAWASILIANO YATOA ELIMU YA ULINZI NA USALAMA MTANDAONI Misalaba Media October 14, 2025 0 Na Tonny Alphonce-Misalaba Media Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,Ofisi ya Rais - Utumishi wametoa elimu ya Ulinzi na Usalama Mtandaoni kwa wanafunzi na walimu wa shule za sekondari za Kilimani na Pamba za jijini Mwanza.Awali akielezea sababu za kutoa elimu hiyo Kwa wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu mtalaamu wa Usalama mtandao Yusuph Kileo amesema utafiti uliofanywa unaonyesha watoto wengi wanatumia simu."Utafiti uliofanywa sampling ya watu laki mbili watoto wengi walikiri wanatumia simu,watoto wengine wanatumia simu Kwa kificho na hao watoto walishakutana na changamoto mbalimbali.alisema KileoKileo amesema watoto wakitumia simu vizuri inaweza kuwasaidia kimasomo na hata kubadilishana mawazo na watu wengine.Akizungumza Kwa wakati tofautitofauti na wanafunzi wa shule za sekondari Kilimani na Pamba Kileo amewataka wanafunzi hao kujiepusha na matumizi mabaya ya mtandao ikiwemo kutumia picha za utupu.Nae afisa habari kutoka Tume ya ulinzi wa Taarifa Binafsi Joseline Chambasi amewataka wanafunzi hao kuficha taarifa zao binafsi kwaajili ya Usalama wao."Taarifa zako binafsi ndio wewe ulivyo hivyo kama hakuna ulazima wankuposti mtandaoni tafadhari usifanye hivyo kwasababu mtu alitaka kukufanyia ubaya atapitia kwenye taarifa zako binafsi".alisema Joseline Joseline amewakumbusha pia wanafunzi hao kuhakikisha wanatumia nyira kufungia vitu vyao vya msingi na wasiitoe Kwa mtu mwingine.Akielezea majukumu ya Wizara ya mawasiliano na Teknolojia mwakilishi wa kaimu mkurugenzi wa kitengo Cha ulinzi na Usalama Hafidhi Masoud amesema jukumu la Wizara ya mawasiliano ni kulinda miondo mbinu ya TEHAMA pamoja na mawasiliano yake.Kila mwezi wa kumi Wizara ya mawasiliano na Teknolojia ya habari hufanya maadhimisho ya mwezi wa Usalama mtandao Kwa kutoa elimu Kwa makundi Mbalimbali.Mtalaamu wa Usalama mtandao Yusuph Kileo akitoa, elimu. 🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA You Might Like View all
Post a Comment