Vurugu na uharibifu wa mali wakati wa maandamano ni kinyume na mafundisho ya Maandiko Matakatifu (Biblia), ambayo yanatoa msisitizo mkubwa kwa wajibu wa raia kuheshimu mali na rasilimali.
Taasisi za Dini zinapokosoa Serikali kwa matumizi ya nguvu, hazipaswi kupuuza hatia ya uharibifu wa mali, kwani Kanuni za Mungu zinatambua uwajibikaji huo.
Mchambuzi mmoja wa Kanisa Katoliki, akichambua matamko ya hivi karibuni ya viongozi wa kidini, alieleza kuwa Haki ya Mali ilipuuzwa wakati vifo vilipopewa uzito mkubwa.
Mafundisho ya Biblia Kuhusu Mali na Fidia
Uchambuzi huo wa kiimani unaonyesha kuwa Biblia inatoa usawa wa kina kati ya Haki ya Raia (Uhai) na Wajibu wa Raia (Mali). Aidha anasema Amri ya Nane na ya Kumi inaweka msingi wa kuheshimu mali ya jirani. “Kutoka 20:15: 'Usibebe’ (Usiguse au kuiba). Hii inaenea hadi kwenye uharibifu wa mali au miundombinu,” alisema mchambuzi huyo, akiongeza kuwa hata tamaa ya kutaka uharibifu inakataliwa (Kutoka 20:17).
Wajibu wa Kulipa Fidia: Mafundisho ya Sheria ya Musa yanadai kurejeshwa kwa mali iliyoibiwa au kuharibiwa. “Kutoka 22:6: 'Mtu akiteketeza shamba au mizabibu... atatoa fidia kwa mali iliyoungua.’” Hili linaweka wazi kuwa waandamanaji wa vurugu wanapaswa kutoa fidia kwa uharibifu wowote waliofanya.
Maneno mengi yanayotawanya ni kujaribu kutafuta hisani kwa kuzingatia sana Haki ya Kuishi (Uhai), lakini Haki ya Mali na miundombinu inapuuzwa. Wanaozungumzia hilo la uhai wanaona matumizi ya nguvu ya serikali kama 'uovu mkubwa' kuliko uharibifu wa mali uliofanywa na raia".
Aicha mchambuzi huyo anasema kwamba taasisi za dini zinakosea zinaposhindwa kukemea matamshi ya vitisho kutoka kwa viongozi wa kisiasa ("watakinukisha"). Biblia inakemea matamshi yanayoweza kusababisha uharibifu. Mchambuzi huyo alinukuu Yakobo 3:6: “Na ulimi ni moto... ndio unaotia mwili mzima unajisi, na kuuwasha moto mzunguko wa maisha yetu.” Matamshi ya uchochezi wa vurugu ni sawa na "moto" unaoweza kuunguza jamii.
Anasema Viongozi wa kidini wana wajibu wa kuleta amani. Mathayo 5:9 inasema, "Heri wenye kuleta amani; maana hao wataitwa wana wa Mungu." hivyo kuendelea kutoa sauti za uchochezi kwa jina la kudai haki si sahihi katika muktadha wa kiimani.
Mchambuzi huyo alisema kwamba wakati umefika kwa viongozi wote, wa Serikali na wa Upinzani, pamoja na Taasisi za Dini, kukumbushwa wajibu wao wa kulinda mali na kuepuka uchochezi ili amani ya utaratibu idumu.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
✉️ info@eastafricanspirits.com

Post a Comment