Na: Mwandishi Wetu -
Misalaba Media, DAR
Ni kicheko kwa wanafunzi 66,987 walioomba mkopo wa elimu ya
juu inayoratibiwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB),
ndivyo unavyoweza kusema ndugu msomaji baada ya HESLB kuidhinisha Shilingi
Billioni 215.3 ikiwa ni awamu ya pili ya utoaji wa fedha za kugharamia elimu ya
juu kwa waombaji mbalimbali hapa nchini waliokidhi vigezo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia,
kupitia Taarifa yake kwa Umma aliyoitoa Novemba 7, 2025, katika wanafunzi
66,988 walionufaika na awamu ya pili ya upangaji mikopo na ruzuku, wanafunzi
43,562 ni wa Shahada ya awali na wanafunzi 1,179 ni wa Stashahada ambao kwa
pamoja wamepangiwa mikopo ya Shilingi Billioni 143.7.
Vilevile, wanafunzi 288 wamenufaika na ufadhili wa Samia
Skolashipu, ambapo Shilingi Milioni 575 zimetumika. Sanjari na hao, wapo
wanafunzi 230 wa Shule ya Sheria Tanzania ambao wamefadhiliwa Shilingi Billioni
1.5. Pia, wapo wanafunzi 21,729 wanaendelea na masomo ambao wamefadhiliwa
Shilingi Bilioni 69.4.
Oktoba 24, 2025, Dkt. Kiwia alizungumza na vyombo vya habari Jijini Arusha ambapo alieleza kuwa HESLB imeidhinisha Shilingi Billioni 426.5 kwa wanafunzi 135,240 ikiwa ni awamu ya kwanza ya upangaji mikopo na ruzuku kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo mbalimbali. Huu ni mwendelezo wa HESLB kutoa taarifa juu ya mwenendo wa upangaji mikopo na ruzuku kwa wanafunzi mbalimbali huku wanafunzi hao wakiwa na wajibu wa kurejesha fedha hizo baada ya kuhitimu masomo yao.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment