Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
Watu wengi wamekuwa wakichanganya hizi dhana mbili Soccer School na Academy, ilhali ni vitu viwili tofauti kabisa ndani ya mfumo wa soka la kisasa.
Soccer School ni mahali pa KUJIFUNZIA MISINGI YA MCHEZO WA MPIRA kama ball control, positioning, teamwork, discipline n.k, Hapa mtoto analipa ada ili apate mafunzo bora, vifaa, na exposure.
Mfano, Barça soccer school, PSG Soccer School, na hata Arsenal Soccer School zote wanalipisha Ada kwa sababu zinatoa elimu ya soka kama shule nyingine yoyote.
Lakini Academy, hii ni PROFESSIONAL SETUP YA KLABU(hapa sasa ni baada ya kugraduate na kufanya vizuri kwenye soccer school, Wale vijana wanaochaguliwa humo wanakuwa kwenye talent program ya club, kama akina La Masia ya Barcelona au Manchester City Academy na hawa hawalipi chochote klabu inagharamia kila kitu kwa sababu tayari imewaona kama FUTURE INVESTMENT
Kwahiyo unapokutana na mpango kama Yanga Soccer School, usiuchukulie kama WANAUZA NAFASI hapa jamaa wana invest
Mpira wa kisasa ni sayansi na kama tunataka kuzalisha wachezaji wa viwango vya Samatta, au Feisal, basi lazima tuanze kuwekeza kwenye football education mapema.

Post a Comment