Na Mwandishi wetu, Misalaba Media - Dodoma Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika - Tanzania (Misa - Tan), imewakutanisha wanahabari zaidi ya 100 kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani katika mafunzo ya habari za amani (Peace journalism) hususani nyakati za migogoro.Waandishi hao wamekutana jijini Dodoma leo Novemba 27, 2025, ili kuwawezesha wanahabari kujenga amani kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari.Mafunzo hayo pia yamelenga kuwajengea uwezo waandishi kuelewa dhana ya Uandishi wa Habari za amani, aina ya uandishi unaojikita katika kuimarisha utulivu, kuzuia uchochezi, kupunguza upotoshaji, na kuandika habari zinazojikita kwenye utatuzi badala ya uchochezi.Akifungua mafunzo hayo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Denis Lazaro Londo, amesema waandishi wana jukumu la kulinda umoja wa kitaifa kupitia matumizi ya lugha inayojenga, utoaji wa taarifa sahihi, na kuepuka taarifa zinazoweza kuchochea migogoro, haswa nyakati za migogoro.Amesema waandishi wa habari ni daraja muhimu linalounganisha Serikali na wananchi, hivyo lazima watekeleze wajibu wao kwa uadilifu bila kuyumbishwa na mtu yeyote mwenye nia ya kuichafua tasnia."Tuna imani kwamba mafunzo haya yataleta tija kupitia kwenu wanahabari mliohudhuria, serikali inawahakikishia kuwa mtaendelea kuwa salama na vifaa vyenu wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yenu." Amesema Londo Amewataka wanahabari kutambua kwamba uandishi wa habari ni muhimu lakini uandishi wa habari za amani ni muhimu zaidi, zinazojikita kutunza maslahi ya Taifa na wananchi wake.Amesema wizara ya mambo ya ndani iko tayari kushirikiana na wanahabari katika kulinda misingi ya utawala bora na demokrasia.Amesema serikali inaendelea kuhakikisha wananchi wanapata haki ya kupata taarifa na kwamba falsafa ya 4R inalenga kulinda wanahabari na kutetea uhuru wa kujieleza akitolea mfano wa vyombo vya habari vilivyofungiwa kufunguliwa."Nafarijika kuwa Misa Tanzania mmekuwa mdau mwaminifu kwa serikali katika nyakati nzuri na hata ngumu. Huu ndio uzalendo tunaoutaka kutanguliza maslahi ya Taifa mbele bila kuathiri uhuru wa kitaaluma." Amesema na kuongeza"Wizara ya mambo ya ndani inaendelea kushirikiana nanyi katika mambo yote yanayohusu usalama wa wanahabari, ulinzi wa amani na mafunzo kwa wanahabari katika kuhakikisha kwamba, tunalinda uhuru wa habari, wanahabari wanalindwa, tunatetea uhuru wa kujieleza lakini pia haki ya wananchi wetu kupata taarifa.""Tukio la Oktoba 29,2025 ni funzo kwetu sote, sisi serikali, nyinyi wanahabari na jamii nzima kwa ujumla. Ni kweli wanahabari mnalo jukumu la kulinda amani haki utulivu na umoja wa kitaifa na tunawashukiru sana kwa kuendelea kuhamasisha amani."Akizungumza katika mafunzo hayo, Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko, amesema vyombo vya habari nchini Tanzania havitakubali kuchonganishwa na wananchi bali vitaendelea kusimamia maadili, uzalendo na weledi.Amesema waandishi wa habari ni daraja muhimu linalounganisha Serikali na wananchi, hivyo lazima watekeleze wajibu wao kwa uadilifu bila kuyumbishwa na mtu yeyote mwenye nia ya kuichafua tasnia.“Vyombo vya habari ni nguzo kubwa ya usalama wa Taifa,” amesema Soko. “Hatutaruhusu mtu yeyote kutikisa au kuathiri misingi yetu ya uzalendo. Waandishi wa Tanzania ni wazalendo, si wasaliti”,ameeleza Soko.Akigusia tukio la Oktoba 29, Soko amesema sekta ya habari iliguswa moja kwa moja, kwani baadhi ya waandishi waliumia, walipoteza wenzao na wengine kupoteza vifaa vya kazi.Ametoa wito kwa Wizara ya Mambo ya Ndani kuendelea kulinda amani ya nchi pamoja na kuhakikisha waandishi wanakuwa salama wanapotekeleza majukumu yao.Ameongeza kuwa MISA Tanzania itaendelea kutoa mafunzo ya Uandishi wa Habari wa Amani ili kujenga uwezo wa wanahabari kuandika habari zinazohamasisha amani, kushusha joto la mgogoro, kupunguza taarifa za uchochezi na kuongeza umoja wa kitaifaMhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Alex Sichona amewasihi wanahabari kufanya uandishi wa habari unaochochea amani, kupunguza mifarakano miongoni mwa jamii.Amesema ni vyema wanahabari wakazingatia maadili ya uandishi hususani kwenye vyombo vya habari vya mtandaoni ambavyo wengi wao wamekuwa wakiwahi kutoa taarifa (Breaking News) bila kujiridhisha ama kwa kutumia vichwa vya habari vinavyozua taharuki ili kuvutia wasomaji."Uandishi wa habari wa mtandaoni na mitandao ya kijamii isitumike kukuza migogoro kwa maslahi ya mwandishi na Taifa kwa ujumla. Tusikimbilie kuonekana kwa kwanza kuweka taarifa (Breaking News) bila kujiridhisha vyanzo vya taarifa." Amesema Sichona Amesema kila mwandishi wa habari anatakiwa kuzingatia madhara na faida ya taarifa kabla ya kuitoa, kuangalia manufaa yake kwa jamii na kwamba atawajibika kwa jamii yake kwa matokeo ya habari aliyoitoa.Mwisho.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Denis Lazaro Londo, akizungumza wakati akifungua mafunzo kuhusu Uandishi wa Habari wa Amani (Peace Journalism) yaliyoandaliwa na MISA Tanzania
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Denis Lazaro Londo, akizungumza wakati akifungua mafunzo kuhusu Uandishi wa Habari wa Amani (Peace Journalism) yaliyoandaliwa na MISA Tanzania
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Denis Lazaro Londo, akizungumza wakati akifungua mafunzo kuhusu Uandishi wa Habari wa Amani (Peace Journalism) yaliyoandaliwa na MISA Tanzania
Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko, akizungumza.



🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254









Post a Comment