Na Lydia Lugakila, Misalaba Media Wazazi na walezi wa watoto wanaosoma katika Shule ya Lwekebu Day Care iliyopo Iwambi, mkoani Mbeya, wamepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Mkurugenzi wa shule hiyo, Bupe Mdong’ara, kwa kutoa malezi na elimu bora kwa watoto wao.Wazazi hao, akiwemo Bi. Ester Landulila, Leonia Mahenge, Espina Manika, Angel Hansi, Dorcus Berdoni na Devotha, wametoa pongezi hizo wakati wa mahafali ya tatu ya shule hiyo yaliyofanyika Novemba 25, 2025.Wamesema kuwa wanatambua mchango mkubwa unaotolewa na mwalimu Bupe, hususan katika kuwalea watoto katika maadili mema na kuwatengenezea msingi mzuri wa kielimu. Wazazi hao wamebainisha kuwa malezi mazuri yanayotolewa shuleni hapo yamewavutia hata kuwaleta watoto wao wengine kujiunga kwa awamu zinazofuata.Akisoma risala ya shule, Mkurugenzi Bupe amesema kuwa Lwekebu Day Care ilianzishwa mwaka 2022 ikiwa na watoto 18 pekee ambapo tangu hapo, kituo kimeendelea kushuhudia ongezeko kubwa la wanafunzi kila mwaka sambamba na ufanisi mzuri wa watoto wanaoendelea kujiandaa kuingia darasa la kwanza.Bupe amebainisha kuwa kituo kinatoa huduma za daycare na elimu ya awali kwa watoto kuanzia umri wa miaka miwili, kwa lengo la kuwaandaa kuwa na misingi imara ya kimasomo na kimaadili.Pamoja na mafanikio, Bupe ametaja changamoto kadhaa zinazoikabili shule hiyo, ikiwemo upungufu wa vitabu vya kiada na ziada, pamoja na vifaa vya michezo vinavyohitajika kwa ajili ya kukuza ujuzi na ubunifu wa watoto.Kwa upande wake, mgeni rasmi katika mahafali hayo, Bi. Joyce Yosam Mwampamba, amempongeza Mkurugenzi Bupe kwa kazi nzuri anayofanya katika kutoa huduma nzuri na malezi yenye ubora.Akijibu risala ya shule, Bi. Mwampamba pamoja na timu yake wamekabidhi vifaa vya michezo, vifaa vya kuhesabia na vifaa vya kuchezea, kwa lengo la kuwasaidia watoto kujifunza kwa urahisi na kuongeza motisha ya kupenda masomo.Aidha, amewakumbusha wazazi na walezi kuhakikisha wanawafuatilia watoto wao katika tabia, mienendo na masomo, ikiwemo kuwahimiza kufanya kazi ya nyumbani(Homework) wanapoelekezwa na walimu wao, ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao za baadaye.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254















Post a Comment