" MKUTANO WA 26 WA TEKNOLOJIA YA DAWA NCHINI WAFANYIKA MWANZA.

MKUTANO WA 26 WA TEKNOLOJIA YA DAWA NCHINI WAFANYIKA MWANZA.

Na Mwandishi wetu, Misalaba Media Chama Cha Wateknolojia Dawa Tanzania (TAPHATA) kwa kushirikiana na vyama vingine vya kitabibu wamekutana katika mkutano wao wa 26 Jijini Mwanza kujadiliana namna ya kuboresha huduma za kitabibu nchini ziweze kuwa na mafanikio.Rais wa TAPHATA Thabit Milandu alisema lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha watalaamu wa nyanja za tiba nchini kwa lengo la kubadilishana uzoefu, ujuzi, kufanya mafunzo na kutoa tuzo kwa walioonesha mafanikio ya teknolojia ya tiba hapa nchini ili kuwezesha kuwepo kwa mafanikio na maboresho makubwa yatakayochochea ukuaji wa sekta ya tiba hapa Tanzania.Aidha Milandu alisema kuwa kila mwaka TAPHATA pamoja na vyama vingine vya kitabibu hukutana kwa lengo la kubadilishana maarifa, uzoefu na kuangalia changamoto zinazojitokeza ili kuzitafutia ufumbuzi wenye tija ambapo kwa mwaka huu washiriki zaidi ya 1000 wamehudhuria katika kongamano hilo liloanza tarehe 26 likitarajiwa kumalizika Novemba 28.Alisema mwaka huu kongamano lao limepambwa na kauli mbiu isemayo "Kuwezesha Wateknolojia Dawa, kubuni na kuendeleza mustakabali wa Teknolojia ya Dawa Nchini Tanzania -Dawa salama, Taifa salama".
Milandu alisema vilevile suala jingine ambalo wanalipa kipaumbele ni kuangalia namna gani ya kuhakikisha kuwa wagonjwa wanapata dawa salama na mgonjwa kwenye hospitali za serikali hakoswi dawa ya matibabu.Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda aliwataka Wateknolojia dawa kutokuvunjika moyo kutokana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwani fani yao inawaruhusu kujiajiri wenyewe na serikali inaweza kuwapatia mikopo ya kuendeshea shughuli yao.Alisema kazi ya Wateknolojia dawa inahitaji wito hivyo uzingatiaji wa miiko ya kazi zao ni mhimu katika utoaji wa huduma kwenye jamii hivyo kwa ambao hawajapata ajira waombe kazi katika sekta ya afya kwani serikali ilitangaza nafasi za ajira zaidi ya 10,000.Msajili Baraza la Famasi, Boniface Magige alisema lengo la kongamano hilo ni pamoja na kuwakumbusha watumishi hao kuzingatia utaratibu wa maadili ya kazi zao kama inavyowataka kwenye utendaji kazi zao za kila siku.Alisema bajeti kwa ajili ya ununuzi wa dawa hufanywa kwa nchi nzima ambapo usambazaji hufanywa kwa haraka ili kufika sehemu husika na kutoa onyo kwa wale ambao hujinufaisha wenyewe kwa uuzaji wa dawa zinazotolewa na serikali.Naye Mteknolojia Dawa Mwandamizi, Janeth Kipanda alisema katika kuhakikisha kuwa wagonjwa wanapata dawa salama kwa afya zao huteketeza dawa zisizo salama katika maeneo mbalimbali hapa nchini wanapobaini.Alisema serikali imekuwa ikihamasisha kutengeneza dawa zake na vilevile kuwatia moyo wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kujenga viwanda ili kufanya bei ya bidhaa hiyo kuwa chini hivyo kuwezesha watumiaji kumudu gharama zake.Mfamasia toka Bohari ya Madawa (MSD), Mussa Sayyida alisema zaidi ya asilimia 90 ya dawa mhimu zinapatikana hapa nchini na fedha zipo za kuwezesha usambazaji wake muda wowote.Alisema serikali imewekeza kiasi kikubwa katika kuhakikisha kuwa inakuza teknolojia ili kuwezesha dawa hizo kuzalishwa hapa nchini.Sayyida alitaja viwanda vya kutengeneza dawa vinavyomilikiwa na serikali kuwa ni Idofe pharmaceutical kilichopo Makambako, Keko Pharmaceutical na Arusha Pharmaceutical huku vya watu binafsi ni Kairuki Pharmaceutical, Shelly's pharmaceutical na Zenafa pharmaceutical.

 


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post