" MWENYEKITI WA DAYCARE MBEYA ATOA WITO KWA WAZAZI KUWAANDIKISHA WATOTO KATIKA SHULE BORA, AITAJA MBEYA BRIGHT STARS DAYCARE AND PRIMARY KUWA CHAGUO SAHIHI

MWENYEKITI WA DAYCARE MBEYA ATOA WITO KWA WAZAZI KUWAANDIKISHA WATOTO KATIKA SHULE BORA, AITAJA MBEYA BRIGHT STARS DAYCARE AND PRIMARY KUWA CHAGUO SAHIHI

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media- Mbeya

Mwenyekiti wa Umoja wa Daycare Mbeya, Salome Isack kutoka shule ya Mbeya Bright Stars Daycare and Primary iliyopo Lumbila, Iwambi Mkoani Mbeya, ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao shuleni hapo kutokana na ubora wa elimu na huduma zinazotolewa.

Akizungumza katika mahafali ya kituo cha Lwekebu Day Care, Salome Isack amewashauri wazazi na walezi kuwapeleke watoto wao Mbeya Bright Stars, kwani wamejipanga kikamilifu kutoa elimu bora na huduma zinazowafanya watoto kujifunza katika mazingira salama.”

Akiendelea kusisitiza, Bi Salome ameongeza kuwa shule hiyo ina usafiri wa uhakika, chakula cha kutosha na chenye ubora, pamoja na mazingira rafiki kwa ujifunzaji.

“Tunayo huduma ya usafiri iliyo salama, chakula bora kwa ajili ya watoto, na walimu wenye weledi lengo letu likiwa ni kuhakikisha mtoto anapata misingi imara ya elimu na malezi,” alisema Bi Isack.

Aidha, amewahimiza wahitimu wa kituo hicho na watoto wengine kujiunga na Mbeya Bright Stars Daycare and Primary ili kuendeleza safari yao ya kielimu.

“Nawaomba wazazi muwaunge mkono watoto wenu hasa wale wanaohitimu sasa mlione kuwa Bright Stars ni sehemu sahihi ya kuendelea na safari yao ya elimu,” alisisitiza.


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post