" MPINZANI WA YANGA (Js Kabylie) NA RECORDS ZA KUTISHA

MPINZANI WA YANGA (Js Kabylie) NA RECORDS ZA KUTISHA

 Hawa hapa ni Jeunesse Sportive De Kabylie ukipenda waite Les Canaries (Makanali), au Les Lions Du Djurdjura ( Simba wa Djurdjura).

Hawa ndio most successful club in Algeria Kwa mashindano ya ndani na ya nje (Kimataifa) — Wakiwa na makombe 14 ya ligi kuu ya Algeria (Algeria Ligue 1).

Js Kabylie ndio timu pekee kwenye ligi ya Algeria inayoshikiria rekodi ya kutoshuka daraja toka ilivyopanda rasmi msimu wa 1969-70 ikiwa imekaa kwenye ligi kwa mfululizo wa miaka 56.

Kwenye ligi kuu mpaka sasa Js Kabylie wapo nafasi ya 9 wakiwa wamecheza michezo 9 wameshinda 4 wamesare 3 na kufungwa 2.

Wamefunga magoli 11 na kuruhusu 8 huku wakiwa na points 15 pekee kwenye hiyo michezo 9

Kwenye level ya Africa, Js Kabylie ni miongoni mwa timu ambazo zimewahi kuchukuwa makombe ya Caf Champions league, ikiwa na historia ya kubeba  makombe mawili ikiwa ni mwaka 1981 na 1990.

Lakini pia imeshawahi kubeba African Cup Winner's mara 1, Caf Cup imebeba mara 2 na Caf Super Cup mara moja.

Huu hapa ni ushiriki wao kwenye mashindano ya kimataifa kwenye hii miaka 5 ya hivi karibuni: 

Kwenye msimu wa 2020/21 Js Kabylie walishiriki mashindano ya Caf Confederation cup na kufika fainali ambapo walipoteza mbele ya Raja Casablanca.

Kwenye msimu wa 2021/22 walishiriki tena mashindano ya Caf Confederation cup lakini safari hii walishindwa kufuzu kwenda hatua ya makundi baada ya kutolewa na Royal leopard kwenye hatua ya awali

Msimu wa 2022/23 walifuzu kushiriki Caf Champions league group stage na walijikuta wanatoka kwenye haya mashindano baada ya kumaliza wamwisho kwenye kundi.

Msimu wa 2023/24 walishindwa kufuzu kwenye mashindano ya kimataifa baada ya kumaliza ligi wakiwa nafasi 14 na msimu wa 24/25 pia walishindwa kufuzu baada ya kumaliza nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi ya Algeria.

Kiufupi hawa Js Kabylie ni timu inayopambana kurejea kwenye makali yake baada ya kupotea kwenye hii miaka ya karibuni.

Msimu wa 2025/26 wamerejea rasmi kwenye mashindano ya kimataifa na wapo kwenye hatua ya makundi, wakiwa kwenye kundi linaloundwa na timu za Al Ahly, Far Rabat na Yanga.

Next stop kwa Yanga ni dhidi ya hawa Js Kabylie siku ya ijumaa pale Algeria.


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post