" MR. BLACK ACHUKUA FOMU KUGOMBEA NAFASI YA SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MR. BLACK ACHUKUA FOMU KUGOMBEA NAFASI YA SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


 Peter Alex Frank, anayefahamika kama Mr. Black, kutoka Shinyanga Mjini, leo amechukua na kurejesha fomu ya kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Makao Makuu ya CCM Taifa, jijini Dodoma.

Mr. Black ni mmoja wa watia nia waliowasilisha fomu zao rasmi leo Tarehe 04, 11, 2025, na ameahidi kwamba endapo atapata nafasi hiyo, atatumia uwezo na uzoefu wake kulinda na kusimamia kanuni, sheria na taratibu za Bunge, pamoja na kuimarisha uwajibikaji wa wabunge katika majimbo yao ya uwakilishi.

Ameeleza kuwa ataendesha Bunge kwa weledi, hekima na mbinu za kisasa, akilenga kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu ya Bunge kwa maslahi mapana ya Taifa.

Mr. Black amewahimiza Watanzania wote kumuombea ili kufanikisha dhamira yake ya kulitumikia Taifa kupitia nafasi hiyo.


Post a Comment

Previous Post Next Post