" EDWIN SOKO AWAASA WAANDISHI WA HABARI KUTOKATA TAMAA

EDWIN SOKO AWAASA WAANDISHI WA HABARI KUTOKATA TAMAA

Mwandishi wa habari Mwandamizi na mtetezi wa haki za binadamu Edwin Soko  amewaasa waandishi wa habari kutokata tamaa licha ya kupitia changamoto za kikazi walipokuwa wakitimiza majukumu yao kwenye uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akizungumza na Msalaba Media Soko  amesema kuwa, kuna  baadhi ya waandishi wa habari wamepata madhila wakati wakitimiza  majukumu yao hali hiyo isiwafanye wakate temaa na kujutia kuwa waandishi wa habari.

"Kila kazi Ina changamoto yake hivyo kuwa Mwandishi wa habari ni wazi kukubali kufanya kazi ya  kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha jamii hivyo basi ni lazima kuzikubali changamoto zote tunazokumbana nazo kwenye kutafuta na kutoa taarifa ili kulijenga Taifa letu"amesema soko

Aidha  ametoa pole kwa baadhi ya waandishi wa habari waliopata madhila na watanzania wote kwenye mchakato mzima wa uchaguzi wa Oktoba 29, huku akiwasahii   waandishi wa habari  kuendelea kuitumikia fani hiyo bila kukata tamaa.

 Ameongeza kuwa, katika nyakati zote ziwe ngumu au nyepesi waandishi wa habari wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi na kulinda maslahi ya Taifa


Post a Comment

Previous Post Next Post